Mkuu wa mkoa wa Arusha aiagiza Halmashauri ya Monduli kupitia upya kanuni zilizotumika kwenye umiliki wa Manyara Ranch
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo akihutubia wananchi wa kijiji cha Esilalei katika tarafa ya Makuyuni Wilayani Monduli |
Mkurugenzi
Mtendaji wa AWF akisoma taarifa fupi ya mradi wa shamba la Manyara
Ranch kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(hayupo pichani),pembeni
yake (kulia) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega
akifuatilia taarifa hiyo.
|
Wananchi wa kijiji cha Esilalei wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa Makuyuni alipofanya ziara katika tarafa hiyo iliyopo Wilayani Monduli. |
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza
halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kupitia upya taratibu na kanuni
zilizotumika kwenye umiliki wa shamba la Manyara Ranch lililopo tarafa ya
Makuyuni.
Alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja katika tarafa
hiyo nakutembelea shamba la Manyara Ranch ambalo wananchi wanadi ni mali yao
baada ya umiliki wake kufutwa mwaka 1999 nakurudishwa kwa wananchi.
Hata hivyo bado kuligubikwa na maswali mengi ya hati
miliki ya shamba kuandikwa jina la Tanzania Land Conversation Trust (TLCT) ambacho ni chombo cha kusimamia shamba hilo
na badala ya mmiliki mkuu ambae ni Halmshauri ya Wilaya ya Monduli, hali iliyopelekea
Gambo kutolea maamuzi ya hati miliki iandikwe Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
“Naiagiza Halmashauri kuhakikisha hati miliki ya shamba
hili isomeke jina la Halmashauri badala ya TLCT kwasababu tayari shamba
lilisharudishwa kwa wananchi na halmashauri ndio msimamizi wa mali za
wananchi”,alisema.
Akisoma taarifa fupi ya shamba la Manyara Ranch
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya African Wildlife Foundatio(AWF)ambao ndio
wanaendesha shughuli zote katika shamba hilo bwana Fidelisi Ole Kashe amesema
taasisi hiyo iliingia mkataba wakuendesha shughuli zote ndani ya shamba kutoka
kwa TLCT baada ya chombo hicho kushindwa kuziendesha.
Aidha akifafanua zaidi Mkurugenzi mtendaji wa TLCT bwana
Boniface Ngimojiro alisema TLCT iliundwa na bodi ya halmashauri ya wilaya ya
Monduli ili isimamie na kuendesha shughuli zote za shamba la Manyara Ranch na
baada yakushindwa kuendesha ndipo wakazikabidhi kwa AWF.
Hata hivyo Gambo alisema ataunda timu yakuchunguza
shughuli zote za TLCT kwa mda wa miaka 10 ya nyuma ilikusaidia kufahamu zaidi kama
chombo hicho bado kinahitajika katika uwendeshaji na usimamizi wa shughuli za
shamba la Manyara Ranch.
Gambo amekuwa akifanya ziara zake katika wilaya
mbalimbali za Mkoa wa Arusha kwa lengo lakusikiliza kero mbalimbali za wananchi
zinazowakabili.
No comments