Polisi Dar yasaka mtandao unaotoa mafunzo ya kigaidi kwa watoto
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia wanawake wanne
na watoto minne wanaofundishwa uhalifu wa kutumia silaha na mbinu za
kigaidi katika kambi zilizomo kwenye misitu ya pori la Vikindu.
Kamishna
wa Kanda hiyo, Simon Sirro amesema kikosi cha kupambana na uhalifu wa
kutumia silaha na ujambazi cha kanda hiyo, kilifanya operesheni katika
msitu huo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Kamanda
Sirro ameeleza kuwa awali Polisi walipokea taarifa toka kwa mzazi wa
kiume aliyefahamika kwa jina la Shaban Abdallah Maleck mkazi wa Kitunda
kuwa ametoroshewa watoto wake wanne na mtalaka wake aitwaye Salma
Mohamed anayetuhumiwa kuingizwa kwenye harakati za kigaidi.
Na kwamba baada ya taarifa hizo Polisi walianza kufanya msako katika misitu ya pori la Vikindu.
Amesema
kuwa, baada ya watuhumiwa kuhojiwa imedhihirika kuwa watoto hao
wameachishwa masomo na kuingizwa katika madrasa ambazo ndizo kambi
walizokamatwa chini ya uangalizi wa wanawake.
Amesema
watoto hao hufundishwa mbinu za mapigano, namna ya kutumia silaha
pamoja na kufunzwa kupora au unyang’anyi kwa kutumia silaha.
Pia hufundishwa kujenga uadui na Polisi, walinzi katika taasisi za fedha, na makafiri.
Aidha,
Kamanda Sirro amesema wanawake hao wanaendelea kufanyiwa mahojiano ili
kuweza kubaini mtandao mzima ili kutokomeza tabia ya kufundisha watoto
uhalifu hususani kwamba wanaochukuliwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka
minne na kuendelea.
No comments