Samia Suluhu:Nchi za Afrika zatakiwa kuruhusu watu binafsi na mashirika binafsi kupeleka kesi mahakama ya Afrika
Makamu wa rais Samia Suluhu
Na Vero Ignatus Arusha
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania
Samia Suluhu, amezitaka nchi zilizosaini mkataba wa kulinda na kutetea
haki za kibinadamu ziruhusu watu binafsi na mashirika binafsi kupeleka
kesi mahakama ya Afrika.
Amezungumza hayo wakati akifungua mkutano wa 5 wa
demokrasia, haki za binadamu na utawala bora, amesema ni wakati sasa wa
nchi hizo kuiga mfano kutoka nchi ya Tanzania kwa kuwaruhusu wananchi
wake pamoja na mashirika binafsi kufungua kesi kwenye mahakama ya afrika
Awali, amesema licha ya Afrika kuanza kuwa na muitikio
mkubwa kwenye maswala ya utetezi wa haki za kibinadamu, kwa nchi ya
Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuitikia matamko pamoja na kuyatekeleza
maswala ya haki za kibinadamu kutoka kiwango cha mataifa hadi kufikia
wananchi.
.
"Tumefungua taasisi na vyombo mbalimbali vinavyoshughulia
utetezi wa haki hasa haki za binadamu, haki za wanawake na haki za
watoto na tumehakikisha kuwa kila mwananchi haki zake za msingi
anazipata na kuzilinda, "alisema Samia Suluhu
"Kwasasa tumehakikisha watu wote wanapata haki ya elimu, ndio mana kuna elimu bure, haki ya maisha, haki ya kupata makazi,
Kwa upande wa haki ya Afya, alisema Tanzania ipo katika
mchakato wa kuongeza bajeti yake kufikia 10%, ikiwa ni kuitikia amri ya
tamko la Abuja lililotaka bajeti ya Afya kwa nchi za Afrika ifike
asilimia 15%
Pia amesema licha ya Tanzania kufanya vizuri kwenye utetezi
na ulindaji wa haki zawanamke pamoja na kumuwezesha kushiriki kwenye
ngazi zote za maamuzi,idadi ya ushirikishwaji wa wanawake kwenye bodi za
maamuzi kwenye sekta binafsi bado ni changamoto
"Kwasasa kuna benki ya wanawake inayotoa mikopo kwa
wanawake kwaajili ya kuwawezesha kiuchumi, naomba nitoe wito kwa benki
binafsi zitenge pesa wanawake kwaajili ya kuwakopesha, "alisema Suluhu
Kwa Upande wa jaji Mkuu wa nchi, Othman Chande, alisema
kitendo cha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 7 zilizoruhusu, wananchi
kifungu kesi na mahakama ya Afrika, watanzania wengi wamejitokeza
kufungua kesi kwenye mahakama hiyo
" Kuruhusu wananchi kufungua kesi kwenye mahakama ya Afrika
ni moja ya chachu ya kusaidia utekelezaji wa haki za kibinadamu,
"alisema Jaji Chande
Rais wa Mahakama ya Afrika Silvia Ore, pia alisema kuruhusu
kufungua kesi kwenye mahakama hiyo si mbaya kwakua ni moja ya mikakati
ya kuhakiki haki za kibinadamu zinalindwa na kutetea.
No comments