Mahakama kuu mkoani Arusha yatupilia mbali ombi la lema la kufanya marejeo,mawaklili wake waahaha kukata rufaa,Lema arudishwa mahabusu
| Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatoka mahakamani jana .Picha na Vero Ignatus Blog |
| Baadhi ya wananchi wa Arusha wakiwa nje ya mahakama hapo jana .Picha na Vero Ignatus Blog. |
Na.Vero Ignatus.Arusha.
Mahakama kuu mkoani Arusha imetupilia mbali ombi la mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema la kutaka kufanya marejeo ya uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi ya kusimamisha keshi inayomkabili kutokana na pingamizi la dhamana lililowekwa na upande wa jamuhuri.
Akitoa uamuzi huo wa mahakama jaji anayesikiliza kesi hiyo Sekela Moshi amesema kuwa baada ya kupitia hoja za pande zote mbili amebaini kuna mapungufu hivyo ametupilia mbali hivyo mshtakiwa anayo nafasi ya kukata rufaa.
"Nakataa ombi la kufanya marejeo naamuru hivyo"alisema Jaji Sekela.
*******
Hili ni jaribio lingine la mbunge huyo wa Arusha mjini la maombi ya dhamana baada ya kukamatwa novemba 3 akitokea dodoma na kuendelea kusota mahabusu.
Godbles Lema anatuhumiwa kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ombi hilo la dhamana linakwama tena kwa mara nyingine ya tatu sasa.
Wiki iliyopita mbunge huyo ilishindikana kupatiwa dhamana baada ya kuzuka malumbano ya kisheria kati ya upande wa Jamhuri na mawakili wa Lema .
Baada ya malumbano hayo mahakama kuu kanda ya Arusha ilipanga kutoa uamuzi kuhusu hoja za Jamhuri kupinga mapitio ya kesi hiyo.
Na Kaimu Jaji mfawidhi Sekela Moshi alitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza piungamizi mbili hizo za mapitio ya shauri hilo zilizowasilishwa na mawakili wa Jamuhuri na wale wa lema.
Lema anatetewa na mawakili Peter Kibatala,John Mallya,Adam Jabir,Faraja Mangula,Charles Adiel,Sheck Mfinanga.
No comments