Wataalam wataka makaburi ya albino kulindwa
Mtaalam wa maswala
ya watu wenye ulemavu wa ngozi ameambia BBC kwamba miili ya watu hao
iliozikwa inendelea kufukuliwa kwa lengo la kuchukua viungo vyao.
Zaidi ya albino 600 wameuawa katika mataifa tofauti nchini Afrika tangu mwaka 2007 kutokana na mila potofu.
Sasa mtaalamu huyo Ikponwosa Ero anasema kuwa miili iliozikwa pia inalengwa.
Alikuwa akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika kando kando ya mji wa Nairobi ambao uliwaleta pamoja wawakilishi kutoka mataifa 15.
Visa vingi vimeripotiwa nchini malawi,Mozambique na Tanzania ambapo albino wengi wanashambuliwa sana.
Waliohudhuria wametaka makaburi ya albino kufunikwa na saruji ili kuzuia ufukuaji.
No comments