ESRF yazindua mpango mkakati wa miaka mitano wa utafiti


Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imezindua MPANGO Mkakati wa miaka mitano 2016 – 2020 ambao umeainisha vipaumbele saba kwa kufanyia Utafiti katika masuala mbalimbali ya Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo  jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shabani kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James.

Mpango Mkakati huo  2016 – 2020 ambao ni wa sita tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo,umeainisha maeneo makuu saba  ambayo ndani ya maeneo hayo kuna maeneo mengine madogo madogo ishirini na sita ambayo kwa pamoja  yatatiliwa mkazo katika kipindi hicho cha miaka mitano.

Maeneo hayo makuu ni; Kukuza Uchumi, Ajira na Viwanda; Utawala na Uwajibikaji; Utandawazi na Ushirikiano wa kikanda; Utoaji wa huduma na ulinzi wa kijamii; Mali asili na Usimamizi wa Mazingira;  Usimamizi wa Maarifa na Ubunifu pamoja na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu.
img_8446Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (wa pili kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za ESRF kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF kuzindua Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020. Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kushoto) pamoja na Mshehereshaji wa uzinduzi wa mpango mkakati huo, Prof. Samuel Wangwe (wa pili kushoto).

Bi. Amina alisema kwamba serikali imefurahishwa sana na juhudi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
 kusaidia serikali kusukuma mbele huduma zake kwa jamii na kupanua uwezo wa kutengeneza Taifa  linalotekeleza sera za ukuaji wa uchumi.

Aliwapongeza waandaaji wa Mpango Mkakati huo na kusema Wizara yaFedha na Mipango inafurahishwa sana na namna Taasisi hiyo kama chombo cha Utafiti  kinavyosaidia  kuonyesha  njia na kutoa mwelekeo kwa masuala mbalimbali ya kisera na utekelezaji.
img_8464Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) akiongozana na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na Mpango Mkakati huo, serikali imefurahishwa  kuona kuwa taasisi hiyo pia imejikita katika kusaidia kuona serikali inafanikisha utekelezaji wa maendeleo endelevu nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akizungumza kabla ya kumkarisbisha mgeni rasmi Bi. Amina  kuzindua Mpango Mkakati huo pamoja na mambo mengine alisema kwamba Taasisi yake imejikita katika kufanya tafiti  maeneo saba ambayo yamo katika mpango wa pili wa maendeleo.

Wadau katika kujadili Mkakati huo wameiomba  Serikali kufanikisha Tafiti zote zilizokusudiwa kufanywa zinatekelezwa  kwa kuisaidia Taasisi.
img_8492Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida akizungumza machache na kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.
img_8532
img_8576Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James kwenye uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
img_8639Sehemu ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika hafla ya uzinduzi huo.
img_8655Mtafiti Mshiriki Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Oswald Mashindano akielezea wadau mbalimbali mambo muhimu yaliyomo katika mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
img_8611Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akikata utepe kuzindua rasmi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) wakishuhudia tukio hilo.
img_8620Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) kwa pamoja wakiwa wameshika mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 mara baada ya kuuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
img_8695Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 wakipitia mpango mkakati huo uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.
img_8714
img_8728Sehemu ya wadau, wageni waalikwa na wafanyakazi wa ESRF katika hafla hiyo ya uzinduzi.
img_8524
img_8647
img_8757Pichani juu na chini ni wageni waalikwa walioshiriki kwenye uzinduzi huo wakitoa maoni juu ya mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020  mara  baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
img_8789
img_8930Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango mkatiti huo.
img_8721MC ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya ufundi inayotoa ushauri kwa menejimenti ESRF, Prof. Samuel Wangwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF, jijini Dar es Salaam.img_8937Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
img_8953Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango mkatiti huo.

No comments