Urefu wamsababisha kushindwa kupata matibabu
Baraka Elias
Mashauri, ni kijana Mtanzania mrefu wa futi 7.4, urefu wake usio wa
kawaida umemfanya kushindwa kupata matibabu ya kubadilishiwa nyonga
baada ya kuanguka nyumbani kwake.
Elias alipelekwa kwenye Taasisi ya tiba ya mifupa ya Muhimbili, MOI kwa ajili ya uchunguzi wa madaktari, akitokea mkoa wa Ruvuma kusini mwa Tanzania, baada ya kukosa huduma kwa kile kilichoelezwa kutokuwa na wataalam na vifaa vya kumtibu.
''Madaktari wa MOI wamesema kuwa vifaa walivyonavyo na wagonjwa waliozoea kuwahudumia ni tofauti na mimi," amesema.
"Hata vifaa vya X-Ray haviwezi kutoa picha halisi ya kuona ukubwa wa kifaa wanachopaswa kuniwekea, pia wamesema vitanda vya kulaza wagonjwa wakifanyiwa upasuaji ni vifupi kwa kuwa mgonjwa anapaswa mwili wote uenee kitandani''.
Kurithi
Elias amesema jamii inayomzunguka hushangaa urefu wake, lakini anasema kwake anaona kawaida tu kwa kuwa wazazi wake walimweleza kuwa urefu wake ni wa kurithi.''Upande wa familia ya Baba na Mama babu zao wote walikuwa warefu kwa hiyo hii hali nafikiri imesababishwa na vinasaba''.
No comments