KUTOKUZINGATIA VIGEZO KWAKWAMISHA RUFAA YA LEMA
| Wananchi wa Arusha wakiwa mahakamani siku ya jana.Picha na Vero Ignatus Blog. |
| Wafuasi wa chadema wakiwa wamevalia tshirt zilizoandikwa Justice 4 Lema mahakamani jana.Picha na Vero Ignatus Blog. |
| Watu wakiwa nje ya maakama jana .Picha na Vero Ignatus Blog |
| Na .Vero Ignatus Arusha. |
| |||
Upande wa jamhuri waweka pingamizi juu ya rufaa hiyo iliyokatwa ya kusikiliza pingamizi ya uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi juu ya kumnyima dhamana mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.
Akizungumza na waandishi wa habari ,Wakili
mwandamizi Mahakama kuu ya kanda ya Arusha
,Matenus Marando ,alisema wameweka pingamizi la rufaa hiyo kutokana na
upande wa utetezi kushindwa kuzingatia vigezo vya ukatwaji wa rufaa
hiyo
Alisema kuwa vigezo hivyo kwa upande wa
utetezi hawakuonesha nia ya kukata rufaa kwa kuandika notisi ya rufaa na
badala yake walikata rufaa bila kufuata utaratibu huo .
Wakili Marando alisema kuwa kulingana na kifungu cha sheria cha 361(1)(a) cha CPA kilimtaka mkataji
rufaa kuonesha nia ya kukata rufaa kwa kuandika notisi ya rufaa na si
kukata hivyo waliitaka mahakama itupilie mbali rufaa hiyo
""Tulikuja
na pingamizi na tukawapatia upande wa pili baada ya hapo tulienda kwa
jaji Fatuma Massengi ,tumekubaliana kuwa hilo pingamizi lisikilizwe
kwanjia ya maandishi ,"alisema Marando
"Hivyo
tarehe 30 tutawasilisha pingamizi letu saa 2 asubuhi ,saa 6 mchana
upande wa utetezi utajibu ,saa 10 upande wa serikali utajibu hoja lakini
tarehe 2 uamuzi utatolewa na mahakama juu ya pingamizi letu ,"alisema
Marando
"Kama pingamizi letu likishindwa basi
rufaa itasikilizwa na kama litashinda basi watatakiwa tena kukata rufaa
kama sheria ilivyoangiza,
Upande
wa wakili wa utetezi ,Peter Kibatala ,alisema kikubwa kitakachoenda
kubishaniwa ni muda uliotumika kuleta hitaji ya kusudi la kukata rufaa
ambako itaenda kuangaliwa kama ilikuwa lipo ndani ya muda au nje ya
muda.

No comments