Maandamano ya kumpinga Trump yaingia usiku wa tatu
Maandamano yameendelea nchini Marekani dhidi ya Donald Trump katika miji kadhaa ya Marekani kwa usiku wa tatu mfululizo.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Vanderbilt mjini Tennessee, wamekuwa wakiimba nyimbo za uwanaharakati wa kutetea mageuzi na kufunga barabara ya Nashville kwa mda.
Maandamano hayo hata hivyo yalikuwa ya amani huku mengine zaidi yakitarajiwa kuendelea katika jimbo la chicago baadaye leo.
No comments