Hillary Clinton aenda kutembea porini
Mwanamke mfuasi wa chama cha Democratic ambaye alivunjwa moyo na
kushindwa na Bi Hillary Clinton amekutana na mtu asiyemtarajia porini,
mgombea huyo mwenyewe.
Margot Gerster alienda matembezi akiwa na binti yake na mbwa katika msitu wa Chappaqua, New York.Hakutarajia kukutana na Bi Clinton ambaye alishindwa na Donald Trump wa Reublican siku mbili awali, lakini hilo ndilo lililotokea.
Picha yake pamoja na Hillary Clinton ndiyo mara ya kwanza Bi Clinton kuonekana hadharani tangu atoe hotuba ya kukubali kushindwa Jumatano.
Bi Gerster anasema picha hiyo ilipigwa na mumewe Hillary Clinton, Bill.
Ujumbe wake ulipendwa mara zaidi ya 110,000 na kusambazwa na watu 9,000 kabla yake kuufanya wa faraghani.
"Nilimkumbatia na kuzungumza naye na kumwambia kwamba moja ya nyakati ninazojivunia zaidi kama mama ni wakati ambao nilimbeba Phoebe nikaenda naye na tukampigia kura," amesema.
"Alinikumbatia na kunishukuru na tukasemezana na kisha nikamwacha aendelee na matembezi."
Na haionekani kana kwamba hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Bi Gerster kukutana na waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje.
Alipakia mtandaoni picha yake na Bi CLinton, ambaye anasema alipigwa picha naye alipokuwa shule ya pili, wakati wa hafla ya kuchangisha pesa iliyoandaliwa na mamake.
Bi Clinton alikuwa mgeni wa heshima.
About
Products
LIVE TV
Radio
Contact
Friday, 11 November 2016
MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI ARUHUSIWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA
TAIFA YA MUHIMBILI ALIPOKUWA AMELAZWA
Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli leo ameruhusiwa kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kupata nafuu.
- Aidha Mama Janet Magufuli kabla ya kuondoka katika Wodi ya Sewahaji
alipokuwa amelazwa aliwashukuru Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wote
kwa huduma nzuri walizompatia.
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
No comments