RC GAMBO AAGIZA MANYARA RANCHI IREJESHWE KWA WANANCHI,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo akiwasalimiana na viongozi
wa Wilaya katika eneo la mapokezi wakati
wa ziara yake Wilayani hapo.
Meneja wa Ranch hiyo Ndg.
Fidelis Ole Kashe akiwasilisha taarifa ya
Shamba hilo kwenye Kikao maalum na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na
viongozi wa Wilaya.
Mkurugenzi wa TLCT Ndg.
Boniface Ngimojiro akielezea muundo wa Taasisi hiyo yenye umiliki wa Shamba
la Manyara Ranch.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa maelekezo ya kubadilisha Hati ya
Umiliki wa shamba kutoka kwa TLCT kwenda kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei
na Ortukai.
Mbunge wa Longido Mhe.
Julius Kalanga(kulia) akiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika ziara
ya Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo akikagua Boma la Ngombe lililopo katika shamba la Manyara
Ranch.
Eneo la malisho kwa ajili ya Ngombe 780 waliopo katika shamba hilo
na Kondoo 300
Na.Vero Ignarus Monduli.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
ameuagiza uongozi wa wilaya ya Monduli Mkoani Arusha pamoja na baraza la
madiwani la wilaya hiyo kuhakikisha wanabadilisha umiliki wa shamba la Manyara
ranch lenye ukubwa wa ekari 44,930 kutoka kwa taasisi ya Tanzania Land
Conservation Trust{TLCT} kwenda kwa wananchi wa vijiji viwili kama Rais wa
awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa alivyoagiza.
Rc Gambo
alitoa agizo hilo katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata ya
Elesilalei na Makuyuni baada ya kutembelea miradi ya mamilioni ya fedha
iliyopo ndani ya shamba hilo inayofadhiliwa na African Wildlife Foundation{AWF}
na kuelezwa kero na changamoto zilizopo juu ya umiliki wa shamba hilo kwa
taasisi ya TLCT.
Alisema
nyaraka zinaonyesha wazi kuwa Shamba hilo lilitolewa kwa wananchi wa vijiji vya
Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu mwaka 1999 kwa
ajili ya kilimo na ufugaji lakini hilo halikufanyika badala yake taasisi ya TLCT ikajimilikisha shamba hilo
kinyume na maagizo.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema kutokana na hali
hiyo ninawaagiza viongozi wote wa wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa
Wilaya hiyo pamoja na baraza la madiwani kuhakikisha ndani ya muda mfupi
wanabadilisha umilikiwa wa shamba hilo kutoka taasisi hiyo kwenda katika vijiji
hivyo.
Gambo
alisema serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli
iko madarakani kwa ajili ya kuwahudumia wanyonge na watu wa hali ya chini na
kamwe haiwezi kuona baadhi ya watu fulani wananufaika na rasilimali ya nchi kwa
manufaa yao.
Alisema
TLCT inamiliki shamba hilo kinyume na maagizo kwani shamba hilo lilipaswa
kumilikiwa na vijiji hivyo kwa faida yao lakini walijitokeza wataalamu
wakabadilisha maelekezo hayo na
kujimilikisha kitu ambacho Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kulivumilia kamwe.
‘’Nimeagiza
umiliki wa shamba hili unapaswa kubadilishwa haraka kwa kushirikisha vikao na
kufuata taratibu zote za kisheria ikiwemo kupitishwa na baraza la madiwani ili
wananchi waweze kunufaika na ardhi yao na sio watu wachache wanaolipwa
mamilioni ya fedha bila ya sababu za msingi’’alisema Gambo.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Julius Kalanga na Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo Mhe. Isack Joseph wote kwa pamoja waliunga mkono wazo la Mkuu wa Mkoa na
kusema kuwa watatoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha umiliki wa shamba hilo
unabadilishwa na kwenda kwa vijiji hivyo.
Mkurugenzi
wa TLCT Bonfance Ngimojiro alipopewa nafasi ya kujieleza katika mikutano hiyo
miwili alisema kuwa taasisi hiyo inaongozwa na bodi ya wadhamini yenye wajumbe
nane wakiongozwa na Mbunge wa zamani wa Mondul, Mhe. Edward Lowassa kama
mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Ngimonjiro
alikiri kupata amri ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kutoka katika
taasisi hiyo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili lakini yeye hawezi
kujuwa ni kwa nini amri hiyo hadi jana haikutekelezwa.
Mkurugenzi
huyo alisema yeye ni mwajiriwa tu ambaye hajalipwa mishahara kwa miaka zaidi ya
minne sasa katika taasisi hiyo hivyo hawezi kujuwa kwa undani zaidi
kushindikana kutekelezwa kwa amri hiyo kwani wakitafutwa wahusika wanaweza kuwa
na majibu sahihi.
Naye
Meneja wa AWF, Fidelis Ole Kashe yeye alisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi
katika mazingira magumu sana ndani ya shamba hilo pamoja na kufadhili miradi
mbalimbali ya maendeleo katika shamba hilo ikiwemo shule,zahanati ,ufugaji wa
kisasa na machinjio.
Kashe
alisema utulivu ndio njia pekee itayofanya miradi iliyopo katika shamba hilo
kuendelea vinginevyo wafadhili hao wanaweza kusikitisha kila kitu.
Alisema
AWF imekuwa mstari wa mbele kufadhili miradi mbalimbali katika wilaya ya
Monduli na nchini kwa ujumla na inapenda kuona fedha inazotoa zinafanya kazi
iliyokusudiwa na sio vinginevyo.
No comments