Lema ameshindwa kufikishwa mahakamani kutokana na sababu zisizojulikana

Image result for mbunge lema 
Pichani   Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe
Na.Vero Ignatus, Arusha
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye yuko mahabusu ya magereza ya kisongo kwa kukosa dhamana kutokana na kukabiliwa na kesi mbili za jinai, ameshindwa kufikishwa

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye yuko mahabusu ya magereza ya kisongo kwa kukosa dhamana kutokana na kukabiliwa na kesi mbili za jinai, ameshindwa kufikishwa mahakamani kutokana na sababu zisizojulikana 

Kesi hiyo ni kesi nyingine ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa jana akiwa anashtakiwa yeye pamoja na  mke wake kwa kosa la kumtukana mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ,pamoja na kufanya uchochezi 

Akiambia mahakama ,mbele ya hakimu mkazi Augustino Rwezile  , wakili wa serikali ,Fortunatus Mhale ,alisema kushindwa kufikishwa mahakamani kwa mbunge huyo ni kutokana na sababu za kimazingira hivyo aliomba tarehe ipangwe kwaajili ya kusikilizwa kwa hoja ya awali ya kesi hiyo 

Pia ,alisema upande wa Jamhuri hakuwa na makosa kutokana na hati hiyo ya kuletwa mahakamani  ilitakiwa itoke mahakamani kwenda magereza na si kutoka upande wa jamhuri kwenda gerezani 

"Nadhani wakili wa tetezi anachanganya ,si upande wa jamhuri ambao hawakutekeleza amri hiyo bali ni magereza ndio ambao hawajatekeleza amri hiyo ,"Alisema wakili Fortunatus

Pia kutokana na upande wa utetezi wa mshtakiwa kutaka ,upande wa jamhuri kupewa adhabu kwa kudharau mahakama,wakili huyo ,aliiambia mahakama adhabu hiyo ilipaswa kutolewa kwa magereza na si kwa upande wa jamuhuri kwakua magereza ilipaswa kutekeleza amri hiyo 

Hata hivyo ,alisema yeye yuko kwaajili ya kumuwakilisha mkurugenzi wa mashtaka (DPP)  na si upande wa gereza hivyo alitaka hati hiyo ya kumleta mahakamani  iltolewe ili aweze kusomewa hoja za awali 

"Upelelezi umekamilika naomba tarehe ya kusikiliza hoja ya awali itolewe ,"Alisema Fortunatus

Uande wa Utetezi ,wakili John Malya ,aliendelea kuitaka upande wa jamhuri iambie mahakama sababu kamili ni zipi zilizopelekea mbunge huyo kushindwa kufikishwa mahakamani 

Pia kutokana na kuwepo kwa mvutano dhidi ya jamuhuri na upande wa utetezi  ,aliomba mahakama ipange siku ya leo  kusikilizwa kwa kesi hiyo ,ilikuepusha muingiliano wa kesi nyingine ambazo zilikuwa zinamkabili mbunge huyo 

Kutokana na ombi hilo ,Hakimu Mkazi Rwegizile ,alikubali na kutoa amri ya hati ya kumleta mahakamani mbunge huyo itolewe na  mwendesha mashtaka na aletwe mapema asubuhi kwaajili ya kusomewa hoja za awali za kesi hiyo 

Mbunge wa arusha Mjini,Godbless Lema yuko mahabusu kutokana na kukosa dhamana,kutokana na kukabiliwa na kesi ya jinai ya kufanya uchochezi akiwa kwenye mikutano yake ya hadhara kuwa ameoneshwa kama rais Magufuli hatojirekebisha atakufa kabla ya 2020 ,lakini pia yeye na mke wake wanakabiliwa na kesi nyingine ya kumutita Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo "Shoga "Ambako Mke wake alisema alimuita shoga mbunge huyo kuwa ni rafiki yake na si kama alivyochukulia mkuu huyo wa mkoa

Kesi hiyo ni kesi nyingine ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa jana akiwa anashtakiwa yeye pamoja na  mke wake kwa kosa la kumtukana mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ,pamoja na kufanya uchochezi 

Akiambia mahakama ,mbele ya hakimu mkazi Augustino Rwezile  , wakili wa serikali ,Fortunatus Mhale ,alisema kushindwa kufikishwa mahakamani kwa mbunge huyo ni kutokana na sababu za kimazingira hivyo aliomba tarehe ipangwe kwaajili ya kusikilizwa kwa hoja ya awali ya kesi hiyo 

Pia ,alisema upande wa Jamhuri hakuwa na makosa kutokana na hati hiyo ya kuletwa mahakamani  ilitakiwa itoke mahakamani kwenda magereza na si kutoka upande wa jamhuri kwenda gerezani 

"Nadhani wakili wa tetezi anachanganya ,si upande wa jamhuri ambao hawakutekeleza amri hiyo bali ni magereza ndio ambao hawajatekeleza amri hiyo ,"Alisema wakili Fortunatus

Pia kutokana na upande wa utetezi wa mshtakiwa kutaka ,upande wa jamhuri kupewa adhabu kwa kudharau mahakama,wakili huyo ,aliiambia mahakama adhabu hiyo ilipaswa kutolewa kwa magereza na si kwa upande wa jamuhuri kwakua magereza ilipaswa kutekeleza amri hiyo 

Hata hivyo ,alisema yeye yuko kwaajili ya kumuwakilisha mkurugenzi wa mashtaka (DPP)  na si upande wa gereza hivyo alitaka hati hiyo ya kumleta mahakamani  iltolewe ili aweze kusomewa hoja za awali 

"Upelelezi umekamilika naomba tarehe ya kusikiliza hoja ya awali itolewe ,"Alisema Fortunatus

Uande wa Utetezi ,wakili John Malya ,aliendelea kuitaka upande wa jamhuri iambie mahakama sababu kamili ni zipi zilizopelekea mbunge huyo kushindwa kufikishwa mahakamani 

Pia kutokana na kuwepo kwa mvutano dhidi ya jamuhuri na upande wa utetezi  ,aliomba mahakama ipange siku ya leo  kusikilizwa kwa kesi hiyo ,ilikuepusha muingiliano wa kesi nyingine ambazo zilikuwa zinamkabili mbunge huyo 

Kutokana na ombi hilo ,Hakimu Mkazi Rwegizile ,alikubali na kutoa amri ya hati ya kumleta mahakamani mbunge huyo itolewe na  mwendesha mashtaka na aletwe mapema asubuhi kwaajili ya kusomewa hoja za awali za kesi hiyo 

Mbunge wa arusha Mjini,Godbless Lema yuko mahabusu kutokana na kukosa dhamana,kutokana na kukabiliwa na kesi ya jinai ya kufanya uchochezi akiwa kwenye mikutano yake ya hadhara kuwa ameoneshwa kama rais Magufuli hatojirekebisha atakufa kabla ya 2020 ,lakini pia yeye na mke wake wanakabiliwa na kesi nyingine ya kumuita Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo "Shoga "Ambapo Mke wake alisema alimuita shoga mbunge huyo kuwa ni rafiki yake na si kama alivyochukulia mkuu huyo wa mkoa

No comments