AKAA NDANI YA JENEZA KWA SIKU NZIMA ILI SIKU AKIFA ASIWE MGENI WA JENEZA.AMA KWELI DUNIANI KUNA MAMBO!

screen-shot-2016-11-05-at-4-52-30-am
Vera Lucia da Silva mwenye umri wa miaka 44 akiwa kwenye jeneza
wp-1478246299734
akiwa kwenye picha ya pamoja na ndugu zake yeye akiwa amelala kwenye jeneza akiwa hai.
wp-1478246306200
Vera Lucia da Silva Kama anavyoonekana akiwa ndani ya jeneza.
wp-1478246311039

Imetokea nchini Brazil ambapo Mwanamke mmmoja aliyefahamika kama Vera Lucia da Silva mwenye umri wake ni miaka 44 aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili kupata uzoefu wa mazingira halisi ya kifo ili siku akifariki asiwe mgeni na Jeneza.

Vera aliamua kukaa kwenye jeneza hilo akiungwa mkono na familia yake, wakifanya vitu vinavyohusiana na msiba.Vera amesema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote. 

Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 na ilifanyika katika eneo la makaburi.

Inadaiwa kabla ya hayo, ndugu zake walipinga sana na wazo hilo lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho.

No comments