ABEDNEGO HANGO: TUMIENI VIPAWA MLIVYONAVYO ILI KUIJENGA TANZANIA YENYE AMANI NA UPENDO
Na.Vero Ignatus Arusha.
Wito umetolewa kwa watanzania watumie vipaji
walivyonavyo ili kuijenga Tanzania yenye Amani na upendo bila kujali itikadi za
dini wala vyama huku wakijuaya kwamba watu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa
Mungu.
Hayo yamesemwa na muanzilishi na mkurugenzi wa The
worshiperz Abednego Peter Hango katika
hafla ya kumshukuru Mungu kwa mambo
mengi aliyowatendea iliyofanyika katika ukumbi wa New Safari Hotel jijini hapa .
Hango amesema kuwa wameamua kiufanya hafla hiyo kwani
yapo mambo mengi ambayo Mungu amewatendea siyo tu kwa mwaka huu wa 2016 ila
tangia kuanzishwa kw kundi hilo mwaka 2008 ,wakiwa na malengo ya kuwaleta
vijana pamoja wenye shauku ya kumtumikia Mungu,ambapo hadi sasa waapo waimbaji
36 .
Amesema kuwa maono ya kundi hilo ni kuwafundisha na
kuwaleavijana pamoja na waimbaji kwa ujumla ili wawe waabuduo halisi na
wahudumu na siyo kuwa waimbaji pekee jambo ambalo wamefaulu .
Wakati huohuo Kundi The worshiperz wameandaa tamasha kwakushirikiana na
kundi la Gospel Kitaa linalofahamika kama Sifa za Yeriko litakalofanyika hivi
karibuni katika Newlife City Church lililopo mkoani hapa tarehe 9.12.2016.
Tamasha hilo litawashirikisha waimbaji kutoka nchini
Afrika ya kusini,akiwemo Mercy Manqele kutoka kundi la Joyouus
Celebration,Spokazi Nzumalo kutoka kundi la Soweto Gospel Kwaya pamoja na Kgotso
Makgalema kutoka kundi la Spirit of Praise.
Aidha ameainisha waimbaji wakataokuwepo kutoka jijini
hapa ni pamoja na Pcasf,Cahogos,Machalii wa Yesu ,Voice of Joy,na Yusuph
Nahashon



No comments