Joka mwenye sumu kali zaidi duniani huenda akawa jibu la kupatikana dawa ya kupunguza uchungu. Hii ni kwa mujibu ya wanasayansi.
| Joka mwenye sumu kali zaidi duniani 'Blue Coral' |
Joka mwenye sumu kali zaidi duniani
huenda akawa jibu la kupatikana dawa ya kupunguza uchungu. Hii ni kwa
mujibu ya wanasayansi.
Wanasayansi wanasema huenda sumu hii ikatumika kutengeneza dawa ya uchungu. Baadhi ya wanyama ambao sumu yao imetumika kutengeneza dawa ni pamoja na konokono wa baharini na bui bui wa sumu.
Wanasayansi sasa wanataka joka huyu kuhifadhiwa hususan baada ya maeneo mengi anakopatikana kugeuzwa kuwa mashamba ya michikichi. Wanasayansi walifanya utafiti wao katika nchi za China, Singapore na Marekani.
Watafiti wanasema japo kwa mwanadamu nyoka huwa adui, lakini wakati huu huenda akawa suluhu la matatizo mengi ya kiafya.
No comments