FARAJA KOTTA ATAO KAULI KUHUSU MISS TANZANIA 2016 KUANDAMWA MTANDAONI LIVE
Aliyewahi
kuwa mshindi wa Miss Tanzania kwa mwaka 2004, Faraja Kotta Nyalandu
amechukizwa na yale yanayoendelea katika mitandao ya kijamii juu mshindi
wa taji la Miss Tanzania 2016, Diana Edward.
farajaHatua
hiyo imekuja baada ya watu katika mitandao ya kijamii kuanza
kumshambulia mshindi huyo juu ya umri wake. Hata hivyo kamati ya Miss
Tanzania ilitolea ufafanuzi juu ya suala hilo.Miss Faraja Kotta ambaye na yeye pia alipitia kipindi kigumu pindi alipotangazwa mshindi, ameandika ujumbe huu:
"Niliposhinda
Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha
redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo
sikustahili kushinda. Asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya
shindano.
Nilipigiwa simu kuamshwa, nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani,
Nilitetemeka,
nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia.
Niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili. Nilijuta kushiriki
Miss Tanzania.
I
was young and naive. I had just turned 19, coming straight from the
safety nets of Catholic nuns boarding schools. Sikujua kuna watu
wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua.
It
took my parents (RIP) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie
vizuri. I had to dig deep inside me to regain my purpose. I was exposed
to a cruel world and yes, I quickly learnt, it is what it is.
Leo
hii hakuna binadamu mwenye hiyo nguvu niliyompa yule mtangazaji. I
learnt the hard way but I am grateful for the lesson. Thank God I learnt
early. Kuna sehemu ya nguvu niliyo nayo leo iliyotokana na kujeruhiwa
na binadamu na kupona. Lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona,
unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja. Usijitafutie laana za
reja reja.
To the newly crowned Miss Tanzania, Do you honey!
To the rest of us, tujenge zaidi ya kubomoa. Love doesn’t cost a thing!
God bless,
Faraja"
No comments