Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro Kimefanya Tamasha la kuwapongeza wachezaji waliofanya vizuri Afrika ya Mashariki.

Na Vero Ignatus
Kilimanjaro.
Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro kimefanya Tamasha la kuwapongeza wachezaji wa Mchezo huo waliofanya vizuri katika mashindano yaGOJUKAI Karate ya  Afrika yaMashariki
Tamasha hilo limefanyika hivi karibuni katika ukumbi wa shule ya msingi Mrupanga iliyopo katika Wilaya ya Moshi Mjini ,ambapo liliwashirikisha vilabu vya Gojukai Karate vilivyopo Mkoani hapo.
Akizungumza katika Tamasha hilo Mkufunzi mkuu na Mwenyekiti wa Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro bwana Geofrey Kalonga amesema kuwa mashindano hayo yalifanyika mwezi machi 2016 Nchini Uganda ,na kushirikisha nchi tano za Afrika ya Mashariki ambazo ni Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi ambapo nchi ya Tanzania iliibuka kidedea na kutwaa nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake ambaye ni Getrude Gasper Macha na nafasi ya pili kwa upande wa wanaume ilishikwa na Raphael Sangawe.
Aidha Geofrey amesema kuwa changamoto kubwa waliyonayo katika mchezo huo wa Gojukai Karate ni kukukosa wadhamini kama ilivyo kwenye michezo mingine ,Jamii kuuchukulia mchezo huo ni kuwa ni mchezo unaochezwa na watu wahalifu, pia.kukosa sapoti kutoka kwenye Wizara ya michezo.
Mkufunzi huyo amesema kuwa mchezo huo wa Karate unafundishwa kwenye majeshi yote nchini wameiomba serikali kutupia macho macho mchezo huo kwani mchezo huo unaimarisha afya ya ya mwili wa mchezaji, Unajenga nidhamu ya hali ya juu,mchezo huo pia unajenga uwezo wa kujilinda (self defence)
Aidha mchezo huo wa Karate umeingizwa katika orodha ya Michezo ya Olimpiki hivyo kuna haja ya serikali kuwekeza katika mchezo huo kwani ni mchezo unaochezwa na Watanzania na watu wa rika zote na Jinsia zote bila kuwa na madhara ,Pia mchezo huu hauna Ukomo.

Mkufunzi Mkuu wa Gojukai Katare ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro, Sensei Geofrey Cledo Kalonga (pichani) akiwa katika namna ya kusimama iitwayo zenkutsudachi.


Baadhi ya washiriki wa Vilabu vya Gojukai Karate wakiwa katika mazowezi ya pamoja.
Washiriki wa Gojukai Karate wakiwa wanapiga ngumi iitwayo zenkutsu oizuki jodan(kwa lugha ya kijapani) Anayeongoza anaitwa Sensei Hamza Masoud Mzonge ambaye ni msaidizi wa Mkufunzi mkuu wa Karate Mkoa wa Kilimanjaro.



No comments