MFUMO WA USIMAMIZI WA NYARAKA KIDIGITI KUONGEZA KASI YA UTENDAJI SERIKALINI .



Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidigiti
utaongeza kasi serikalini na hivyo kuchochea
maendeleo chanya katika kila nyanja.

Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu Wizara
ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa mafunzo
yanayotolewa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati
walipotembelea mfumo wa usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.

Alisema pia kuwa mfumo huu una faida nyingi na ndio ambazo zimeifanya
wizara hii kutaka kujifunza ni pamoja na suala la gharama na kwa kuwa
serikali ya awamu ya tano iko katika jitihada kubwa za kupunguza matumizi
na kwa kuwa bajeti ya shajala ni kubwa katika taasisi nyingi za serikali hivyo
mfumo huu wa kidijiti utasaidia kupunguza garama kwani hapatakuwa na haja
ya kutumia karatasi na hivyo kupunguza gharama kubwa.

Prof Elisante pia aliongeza kuwa mfumo huu utaongeza usiri wa nyaraka hizi
na kwa sasa zitakuwa zinasomwa na yule tu aliyekusudiwa na kutoa pongezi
kwa ofisi ya rais manejimenti ya umma kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo
huu kwani ukitumiwa vyema utakuwa na manufaa sana.

Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Prof.Faustin Kamuzora alisema kuwa mfumo huo ulijengwa miaka mitatu
iliyopita na unaweza kutumika katika wizara yeyote kwani una ufanisi mkubwa
sana kwani kwa sasa utaweza kuangalia mafaili gani yameingia kwa mfumo
wa kidijitali na kwa namna hii itapunguza garama na muda kwani hatutakuwa
tunatumia karatasi tena.

Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi na Wizara mbalimbali kuwapa elimu ya
kutosha watunza kumbukumbu kwani wao ndio wahusika wakuu wa kwanza
wa mfumo huu na hivyo kuwataka wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na
kuboresha vifaa kama scanner maofisini mwao.

Nae mmoja wa watunza kumbukumbu kutoka wizara Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Bi.Felomena Swai alisema amenufaika na mafunzo hayo na
yatawasaidia katika utunzaji wa kumbukumbu kwani sasa watapeleka barua
kwa wakati na kurahisisha utunzaji wa mafaili.

No comments