ARUSHA: KUTOACHIA TAJI LA MISS TANZANIA

NA VERO IGNATUS  ARUSHA 

Kutokana na Kusimamishwa kwa shindano la umrembo Tanzania (miss Tanzania )
kwa mwaka mmoja imekuwa ni changamoto kubwa kwa waandaaji wa
shindano hilo kwani warembo wengi wamesahau na shindano kwa
ujumla limepungaza motisha.

Hayo yamebainishwa na muaandaaji wa shindano la kumsaka
mrembo wa mkoa wa Arusha kutoka katika kampuni ya Tour Visual
Entertainment Penda Simwita wakati akiongea na mwaandishi wa
habari jana katika kambi ya kumuandaa Miss Arusha.

Alisema kuwa kwa upande wake kumekuwa shindano hili limekuwa
gumu kidogo kwani warembo wengi wamejipweteka na walijisahau
kuwa kunashindano kama hili kwa mwaka huu hivyo ilimlazimu
kutembelea katika vyuo mbalimbali vya hapa mkoani Arusha kwa ajili
ya kuwatafuta warembo ambao watashiriki shindano hili.

"pamoja na kuwa tumewatafuta likini kiukweli tumewapata warembo
wazuri wanasifa na naamini wataweza kutetea taji la miss Tanzania
likatoka hapa kwani wanauwezo na kizuri zaidi najiamini naweza
kuwaandaa maana ata mrembo ambaye anashikilia taji sasa ivi
alitoka mkoa wa Arusha ,na kipindi kile kulikuwa bado kuna mrembo
wa vitongoji kwaiyo alitoka kwangu ambapo niliandaa miss Arusha
City Cetre kwa iyo naamini na uyu atatoka pia kwangu maana najua
kuwapika na kuchagua warembo wazuri wenye sifa heshima na uwezo
pia wanao"alisema Pendo.

Gazeti hili lilizungumza na mmoja wa warembo hao Maurine Ayubu
naye alisema kuwa amefurahi kushiriki shindano hili naanao uwakika
kwa kuwa anasifa zote za kuwa mrembo wa Mkoa wa Arusha,mrembo
wa kanda ya kaskazini na pia anaamini atatetea taji la miss tanzania
libaki Arusha kama linavyoshikiliwa sasa ivi na mrembo wa Tanzania
Lilian kamazima

"nasema hivyo kwakuwa najua urembo najiamini na ninauwezo
kwaiyo naamini nitachukuwa,pia kuna ili swala watu wengi
wamekuwa wakilichukulia na kusema kuwa kuwa miss ni umalaya
nataka niwatoe shaka na niwaambie watu hususa ni wazazi umiss ni
urembo kama urembo mungine na sio umalaya kwani kila mtu
anakuwa na tabia yake ambayo ametoka nayo kwao kwa iyo akifanya
kitu anafanya kama yeye na sio kwamba mrembo akiwa malaya basi
shindano hilo ndio linawafundisha la hasha bali ni tabia ya mtu
binafsi hivyo ata wazazi wasiwazuie watoto wao kushiriki shindano
hili kwa kuwa na dhana ya kuwa shindano hili ni lakimalaya"alisema
Maurine.

Jumla ya warembo 17 kutoka katika mitaa mbalimbali na wilaya
mkoani hapa wanatarajiwa kupanda jukwaani mapema May 28 mwaka
huu katika ukumbi wa Hotel ya Naura Spirng kwa ajili ya kumsaka
mlibwende wa mkoa wa Arusha ambaye atawakilisha mkoa katika
kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania na tukumbuke
mpaka hivi sasa taji hilo la mrembo wa Tanzania linashikiliwa na
Baadhi ya warembo walioshiriki katika kinyang'anyiro cha kumpata Miss Arusha wakiwa katika pozi katika hotel ya Naura Spring iliyopo Jijini Arusha.

Warembo wakiwa wanafanya zowezi la kucheza katika Hotel ya Naura Spring.

No comments