INTERSPORT FC MABINGWA WAPYA LIGI YA KATA.
Neema Mollel Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sakina ambaye pia ni mlezi wa Timu za mpira kata hiyo ya Sakina Jijini Arusha.
Martini Shimweta( Mdau) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Olmatejoo A.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Wilfred Soilel.
Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.
NA VERO IGNATUS ARUSHA.
Timu ya Intersport club yaibuka kidedea katika michuano ya kata nakuchukua kombe kwa kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali iliyofanyika hivi karibuni katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo Jijini Arusha.
Akizungumzia lengo la mashindano hayo Bi Neema Mollel amabaye ni diwani wa CCM Kata ya Sakina ,pia ni Mlezi wa timu hizo amesema kuwa nia ni kupiga vita madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana pamoja,kuwaondoa vijana wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani michezo ni ajira.
Bi Neema amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi Imara ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya kuwatupia lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na jamii.
Akikabidhi kombe kwa washindi ambao ni Interspot club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha ndugu Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga urafiki kati ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia itamfanya kijana ufahamu wake kuchangamka.
Sambamba ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na Tsh 100,000 ,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black Eagle Tsh 50,000.
No comments