Tuesday, May 17, 2016 Kesi ya aliyemtukana Rais Magufuli Facebook imeendelea leo Mahakamani
Kesi inayomkabili Isaac Abakuk ambaye anatuhumiwa kumtukana Rais John
Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook imeendelea leo May 17 2016
kwenye Mahakama Kuu kanda ya Arusha ambapo ushahidi umekamilika na kesi
itaanza kusiklizwa mfululizo kuanzia June 7 mwaka huu.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Augustino Rwezire anayesikiliza kesi hiyo
amesema upande wa mashtaka umekamilisha ushahidi wake na mtuhumiwa
ataendelea na dhamana hadi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa

No comments