Dkt MAGUFULI:PPF NA NCCF KUWEKEZA ZAIDI KWENYE VIWANDA BADALA YA KUWEKEZA KWENYE MAJENGO.
NA VERO IGNATUS ARUSHA.
Jengo la Kitega uchumi la mfuko wa jamii (PPF)lililo zinduliwa.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli alikata utepe katika Jengo la.PPF Jijini Arusha kwa ishara kuwa tayari Limezinduliwa rasmi,Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu wa Bunge,Kazi ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Muhagama, Pia Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango,(wa kwanza kutoka kushoto) ni Meya wa Jiji la Arusha Calisti Lazaro,(wa kwanza kutoka kulia)ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya PPF,Ramadhani Kijah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Urio.( picha zote na Vero Ignatus blog)
Baadhi ya Wananchi Jijini Arusha wakimsikiliza Raisi kwa makini.
Picha ya Pamoja baada ya Jengo la Kitega uchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF)Lililopo Jijini Arusha (picha zote na Vero Ignatus blog)
Rais Dkt.John Magufuli akiwahutubia Wananchi wa Jiji la Arusha .
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ameitaka mifuko ya jamii nchini kuwekeza zaidi kwenye viwanda badala ya kujenga majengo ambayo Watanzania wa kipato cha kawaida hawawezi kupangisha au kufanyia shughuli zake za kila siku.
Ameyasema hayo Jijini Arusha katia uzinduzi wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) ambapo amesema kuwa bora wangeliwekeza zaidi kwenye viwanda ili watanzania wengi wapate ajira na Serikali nayo ipate mapato.
Amesema kuwa mifuko hiyo ya jamii.imekuwa ikichangia pato la Taifa kwa asilimia 12 tu tofauti na nchi nyingine zinachangia hadi asilimia 40 ,huku mhe.rais akiwauliza swali wakurugenzi wa mifuko ya jamii wananchi wa Tanzania watayatumiaje majengo haya? Maana majengo mengi ya mifuko ya jamii hayana wapangaji kutokana na hali halisi ya Mtanzania? alihoji rais swaki ambalo halikuwa na majibu ya haraka.
Ameitaka Mifuko hii ya Hifadhi kuacha mara moja kuwekeza kwenye majengo ,na wawekeze kwenye viwanda ikiwa na nia namalengo ya kumuinua mtanzania mwenye maisha ya hali ya chini,huku akitoa mifano kuwa Tanzania kuna wawafugaji na wanyama wapo hivyo kama wangeliwekeza kwenye viwanda mfano cha ngozi ingelikuwa faida kwa Watanzania wote,Majeshi yote kwani kila mmoja anavaa viatu,hali kadhalika katika kiwanda cha nguo kwani Watanzania wanalima pamba ,badala ya ngozi ,pamba kuuzwa nchi za nje nakuwanufaisha nchi hizo.
Dkt Magufuli ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuwa,waajiri wote ambao hawachangii katika mifuko hii ya jamii ni lazima wachangie kwa kila mfanyakazi ,na michango hiyo.iwasilishwe kwa wakati,pia waajiri wafuate na kuzingatia sheria za kazi na haki kwa wafanyakazi wao.
Hadi sasa mfuko wa wa PPF tayari unawekeza katika majengo yaliyopo maeneo mbalimbali hapa nchini kabla ya jengo lililozindiliwa, mfuko ulifanya uwekezaji mwingine wa nyumba za kuishi (110)zilizopo eneo la Olorieni na Kaloleni ,Hotel ijulikanayo kama East Africa Hotel ambapo ina vyumba vya kisasa 40 ,Pia mfuko umetoa madawati 2000 kwa shule mbalimbali hapa nchini.
Aidha kuhusu mradi uliofunguliwa wa jengo la kitega uchumi upo katika kitalu Na.15 corrido area ambapo ujenzi wake ulianza 2augusti,2013 na kukamilika Dec 2015,jengo lina ghorofa 8 bila kujumuisha eneo la chini (ground floor) jengo hili ni kwaajili ya katumizi yaofisi mbalimbali,jengo.lina nafasi ya kupanga zenye ukubwa wa mitabza.mraba 7549,Ujenzi wa jengo hili umefanywa na kampuni ya Jianching Engineering Company Limited (CRJE),Msanifu Mkuu wa jengo hilo ni Kampuni ya Kitanzania MD ConsultancyLtd,wataalam washauri ni pamoja na Coast Consult (Quantity Surveyors)Undi Campany Ltd(Service Engineer)Tan Consult Ltd(structural Engineer)
Jumla ya gharama za ujenzi wa jengo zilizopitishwa kwa.zabuni ni shilingi billioni 33.91 hadi sasa shilingi shilingi billioni 28.32 zimetumika.kutokana na taarifa za mahesabu ya mradi.Jengo.linatarajia kupata kodi ya pango kiasi cha shilingi bilioni 2.2 bila tozo la ongezeko la thamani kwa mwaka.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa pensheni (PPF) William Urio.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli akisalimiana na Meneja wa Mfuko wa Pensheni (PPF ) Kanda ya Arusha Onesmo Ruhasha.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli akisalimiana na Meneja Mahusiano na masoko wa mfuko wa Pensheni (PPF) Bi Lulu Mengele.
No comments