WIZARA YA SIKITISHWA NA TUKIO HILI.
imesikitishwa na tukio la ubakaji na udhalilishwaji lililofanywa na
wanaume wawili dhidi ya mwanamke mmoja, ambaye alishurutishwa
kuwa mtupu, kufanya ngono bila ridhaa yake, kupigwa picha na
kusambazwa katika mitandao ya kijamii hapa nchini.
Wizara inalaani vikali kitendo hiki cha ukatili na udhalilishaji
kilichofanywa na wanaume wawili, ambao wamekamatwa na Polisi
kwa kuhusishwa na udhalilishaji huo. Mazingira ya ukatili huo
yanahuzunisha, kwani inaelezwa kuwa wanaume hao kwa wakati
mmoja walihusika kumwingilia kimwili pasipo ridhaa yake,
ilihali,wakimpiga picha za tukio zima la ubakaji huo.
Kitendo hiki, ni ukatili usio na kifani, maana kimefedhehesha utu
wake binafsi na kudhalilisha familia yake, na wanawake kwa ujumla.
Aidha, kitendo hiki kinaweza kusababisha madhara makubwa kwa
mwanamke huyukimwili,kisaikolojia, kijamii na kihisia.

No comments