SHAKA AWAWEKA KITIMOTO DC NA MWENYEKITI HANDENI
NA VERO IGNATUS
Mkuu wa wilaya ya Handeni Husna Msangi na Mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya Handeni vijijini Ramadhan Diliwa wamejikuta wakikabiliwa na wakati mgumu baada ya Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka kuwataka wasimame na kutoa maelezo ya kina kufuatia kero zilizolalamikiwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Viongozi hao kwa nyakati tofauti walilazimika kutoaufafanuzi kufuatia kero zilizoelezwa na wana kijiji cha Michungwani kata ya Segera mkoani Tanga.
Katika mkutano huo wa hadhara kabla ya kuhutubiwa na shaka aliwataka wana kijiji kuelezea iwapo wana kero au malalamiko yanayowatatiza katika maisha yao ya kila siku na ambayo hayajapatiwa ufumbuzi .
Mwananchi mmoja mkaazi wa kijiji cha michungwani aliyejitanbulisha kwa jina la Omar Juma Magufuli (45)aliitaka serikali kutoa msimamo kufuatia mvutano uliopo kati wana kijiji na mwekezaji mmoja ambaye wamehidhi ardhi kubwa huku wananchi wakikosa mahali pa kulima.
Juma alisema tatizo hilo kimsingi kwa muda mrefu viongozi wao 2 ameshindwa kulipatia upambanuzi na kulitatua hali inayojenga kizungumuti na kutoelewana kwa muda mrefu.
Asha Hassan (90)pia mkaazi wa kijiji hicho akilaumu kwamba mara kadhaa wanawake wamekuwa wakiunda umoja na ushirika wao lakini hawapati msaada wowote wala viongozi hawapendi kuwaelemisha pamoja na kutopata misaada.
Asha Hassan (90)pia mkaazi wa kijiji hicho akilaumu kwamba mara kadhaa wanawake wamekuwa wakiunda umoja na ushirika wao lakini hawapati msaada wowote wala viongozi hawapendi kuwaelemisha pamoja na kutopata misaada.
Aidha ajuza huyo alitoa shutuma akilaumu mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)kwamba pamoja wanaahidi kusaidia wazee lakini hawatekekezi.
Mwanakijiji mwingine Awesu Rashid alilalamikia kitendo cha hwmkashauri ya wilaya ya Handeni vijijini kuyatoza mabasi madogo yq abiria kila wanapoijgia kwenye stand ya mabasi huku wakiyaacha mabasi makubwa na malori bila kuyatoza ada.
Awesu alisema kinachofanyika si halali na si haki kwani kipato cha wenye mabasi madogo ya abiria hayakishi kulipa ada kila yanapingia stand kwa kila siku.
Wakati wananchi wakimsubiri shama ambaye ndiye mgeni rasmi kutoa maelezo,aliposimama akataka mkuu wa wilaya Msangi asimame mkutanoni na kutoa ufafanuzi kamili kuhusu mvutano uliopo wa ardhi na hatma ya utatuzi wake.
Mkuu huyo wa wilaya aliposimama alikiri kuwa yupo mwekezaji ambaye alinunua ardhi kwa wanakijiji lakini baadaye ikaonekaba shamba hilo liko kwenye mipaka ya kijiji kingine si kile kilichouza ardhi.
"Kwa muda mrefu mzozo huo umekuwa ukitupa shida katkka kuupatia suluhu yake lakini hata hivyo imethbitika kuwepo kwa mikono ya utapeli na ghiliba miongoni mwa watu waliohusika kuuza "alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Handeni vijijini Diliwa akijibu kuhusu utata wa ukusanyaji ushuru wa mabasi madogo na makubwa yakiachiwa bila kutozwa ada,alisema ili mabasi ya mikoani yatozwe ushuru halmashauri uketakiwa kujenga stend bora ya mabasi ambayo itakuwa na vyoo vya uhakika.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa serikali haitaacha kukusanya ushuru kwa ajili ya maendeleo ya jamii na huduma nyingine za msingi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa serikali haitaacha kukusanya ushuru kwa ajili ya maendeleo ya jamii na huduma nyingine za msingi.
Shaka alimshukuru mkuu wa wilaya na mwenyekiti kwa kujua matatizo yaliopo lakini pia kuyashughulikia kwa ukaribu na umakini wa kutosha.
Kaimu huyo katibu mkuu alitoa kadi mpya kwa wanachama wapya wa ccm 80 na umoja wa vijana 30.
No comments