Tiketi Za Treni Kununuliwa Kwa Njia Ya Mfumo Wa Kielektroniki

i
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajia kuanza kutoa huduma ya uuzaji wa
tiketi kwa abiria wanaotumia usafiri wa treni kwa mfumo wa kielektroniki lengo
likiwa ni kuwawezesha wananchi kuweza kurahisha ununuaji wa tiketi hizo na
kupunguza usumbufu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.
Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la nyongeza lililoihusu Wizara
yake ambapo ametaja maeneo ambayo mfumo huo utaanza kufanya kazi ni
pamoja na Mpanda mpaka Tabora, Kigoma mpaka Tabora.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Sabreen Hamza lililotaka kujua
kwanini TRL isianzishe mfumo wa uwakala wa tiketi ili kupunguza adha
wanayoipata wakazi alisema kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri wa
treni katika Mikoa ya Kigoma, uuzaji wa tiketi katika Stesheni ya Reli Kigoma
umekuwa na changamoto kubwa kutokana na ulanguzi wa tiketi.

Amefafanua kuwa, ili kudhibiti ulanguzi huo, Kampuni ya Reli Tanzania iliamua
kubadilisha utaratibu kwa kuuza tiketi siku za safari na kwa kutumiaK
vitambulisho jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ulanguzi wa
tiketi hizo.

Ameongeza kuwa, utaratibu huo umekuwa na changamoto zake kwa
kusababisha wasafiri kulala stesheni au kuwalazimu kuamka alfajiri ili kuwahi
tiketi hizo.

"Ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili si kuanzisha mfumo wa uwakala ambao
utaiongezea TRL gharama za uendeshaji, tatizo kubwa lililopo ni idadi ndogo ya
safari za treni ambapo huduma inayotolewa hivi sasa haikidhi mahitaji halisi ya
wananchi na hivyo kuwa na uhaba wa tiketi kwa abiria", alisema Mhe.
Ngonyani.

Aliongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inatarajia kuongeza
idadi ya treni za abiria kwa njia ya Kigoma ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa
Mkoa huo.
tiket

No comments