Sunday, May 1, 2016 Sherehe za Mei Mosi : Rais Magufuli Ashusha Kodi ya Mapato Ya Mshahara (PAYE) Kutoka Asilimia 11 Hadi 9

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -
PAYE ) kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.

Rais amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake
aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa
kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.

Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi
wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba
mianya yote ya Rushwa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa
wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya
hifadhi ya jamii bila kukosa

No comments