Waandishi wawekwa korokoroni Misri 3 Mei 2016
Mamlaka nchini Misri imeamuru kuwekwa kizuizini kwa waandishi wawili wa
habari kwa wiki mbili, kwa shutuma za kuchochea maandamano.
Wakosoaji wawili wa serikali Amr Badr na Mahmud el-Sakka walizuiliwa kuingia
makao makuu ya waandishi wa habari nchini Misri na polisi waliokuwa
wamevalia nguo za kiraia.
Taarifa kutoka kwa mwendesha mashitaka wa umma inasema waandishi hao
wawili wanashutumiwa kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya
kijamii wakishawishi mashambulizi dhidi ya polisi na wafanyakazi wa jeshi
kwamba wanamiliki silaha za moto.
Muungano wa waandishi wa habari nchini Misri umetoa wito kwa kufukuzwa
waziri wa mambo ya ndani.
No comments