MWANO: SERIKALI ITUPIA MACHO WAWEKEZAJI WA NDANI

Mkurugenzi wa Old East International co.Ltd. Moses Edward Mwano

NA VERO IGNATUS ARUSHA.

Wito umetolewa kwa serikali kuwatipia macho zaidi wawekezaji wa ndani ya nchi,kuwapa ushirikiano wa karibu katika uendeshaji wa viwanda vidogo vidogo,ili waweze kukua zaidi na kufika mbali .

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Old East International co.Ltd iliyopo jijini Dar es salaam, ndugu Moses Edward Mwano, kuwa wanaiomba serikali kuwapa kipaumbele wawekezaji wa ndani ya nchi zaidi  kuliko wawekezaji wageni.

Moses ameiomba serikali na TBS kiweka mikakati wa kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe na viwango vinavyokidhi, kwani kwenye soko kuna bidhaaa feki zinaingia na bei zake ni za chini .

Pia amewataka wananchi wathamini bidhaa zinazozalishwa na wazawa kuliko kushabikia bidhaa za nje ambazo kwa asilimia kadhaa hazina ubora na viwango vilivyo thabiti na mara nyingine zimekuwa zikileta madhara kwa jamii kutokana na kutokuwa na ubora.


Kampuni ya Old East International ambayo ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania, Makao yake makuu yapo Jijini Dar es salaam wanajishughulisha nakutengeneza wino wa Crown Catridges ,pia wanauza mashine za uchapishaji pamoja na kuzifanyia matengenezo,wino huo unatumika katika mashine mabalimbali za uchapaji pamoja na vinakilishi mbalimbali ,hivyo amewataka watanzania wasikimbilie kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi kwani kwa sasa unapatikana hapa nchini kwa bei nzuri nanafuu.

Pia ni kampuni ya kwanza ya Kitanzania ambayo inatengeneza wino huo wa Crowin Catridge, ambapo wameweza pia kuwapatia vijana ajira,amesema changamoto kubwa waliyonayo kwa sasa ni Watanzania wengi wamezowea kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi hivyo wanadhani ya kwamba bidhaa za ndani ya nchi hazina ubora.

Mwano amewataka watanzania kuondoa dhana potofu kuwa bidhaa za ndani ya nchi hazina ubora kama za nje,bali wathamini bidhaa za ndani ya nchi na wawaunge mkono wazawa wenye makampuni ya ndani ambayo yanafanya uzalishaji tena wenye ubora sahihi.

Wino wa Crown Catridge katika muonekano ukiwa kwenye maboksi tayari kwa kumfikia mteja.
Baadhi ya Mashine za Uchapishaji za Kampuni ya Old East International co.Ltd.


Aidha Moses amesema tayari katika Jiji la Arusha yupo msambazaji wa bidhaa za kampuni yao ambapo ni BNZ Technologgy Jengo la Uchumi ghorofa ya kwanza chumba no 107.

No comments