VERO IGNATUS
KILIMANJARO.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick amesema kuwa asilimia 90% ya wafanyakazi hewa Mkoani humu ni waalimu ,ambao pia Kiwango cha elimu imeshuka na kushika nafasi ya 17 Kitaifa jambo ambalo siyo la kawaida.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika sekta zote za Serikali pamoja sekta binafsi ,pamoja na makampuni, yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro, Ambapo mkuu huyo amesema waalimu wengi,mara nyingi hawapo kwenye vituo vyao vya kazi, amesema wengine wamejikita kwenye biashara ya kuendesha bodaboda,na wengine wameingia kwenye ujasiriyama
Mkuu huyo wa mkoa amewaagiza Wakurugenzi kuhakikisha kwamba waangalie waajiriwa wenye sifa za kupandishwa vyeo wafanye hivyo mara moja wakabidhiwe barua zao za kupandishwa vyeo na siyo anapewa taarifa tu bila barua halikadhalika kwa waalimu ambao wamefikia ukomo wa madaraja,amesema kama mfanyakazi atapandishwa daraja na mshahara wake upande kutokana nadaraja husika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick.
Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Waajiri Mkoani Kilimanjaro,watoe mikataba ya ajira kwa wafanyakazi,wa serikalini,Makampuni ,Taasisi mbalimbali, Sekta binafsi pamoja na Mashamba makubwa .
Amesema kuwa kuna baadhi ya Makampuni yamekuwa yakitoa mikataba feki kwa wafanyakazi (Mikataba bubu)ambayo mfanyakazi anasaini bila yeye mwenyewe kuuusoma na kuuelewa,ambapo haki zake za msingi hazipati kama vile Likizo, Matibabu, hazipati kama mfanyakazi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo,Kuhakikisha kuwa mikataba yote ya wafanyakazi inaenda kwenye Ofisi ya Serikali ya Mkoa pamoja na Wilaya ili ipitiwe na Mwanasheria kama ipo sahihi.
Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ya sikukuu ya wafanyakazi mei mosi ya (DHANA YA MABADILIKO m ILENGE KUINUA HALI ZA WAFANYAKAZI) Ni pamoja na waajiri kuwajali wafanyakazi wao wawapo kazini,kujali afya zao, ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
WAAJIRI /Serikalini/Waajiri Binafsi, Wametakiwa kuwaandikisha wafanyakazi wao kwenye MIFUKO YA JAMII,Pia wawakilishe michango ya wafanyakazi wanaowakata katika mishahara yao waiwakilishe kwa wakati katika mifuko hiyo ya jamii ili iwe faida kwa mfanyakazi anapostaafu baadae au kuacha kazi.
No comments