Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makondakaongeza siku za bure kupanda Mabasi yaHaraka .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi
wa habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata
Kariakoo leo, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za
mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa.
Pia amewaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na
maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa
mabasi ya mwendo wa haraka.
Amesema ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa
watumiaji wa mabasi hayo kwaajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata
tiketi na jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwaajili ya kusubiri
magari.
No comments