Tuesday, May 3, 2016 .Kesi Kitilya na Wenzake Yaahirishwa tena mpaka Mei 18

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam inatarajia kuanza
kusikiliza rufaa ya kupinga kufutwa shtaka la nane katika kesi inayomkabili
aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry
Kitilya na wenzake wawili, mei 5, mwaka huu.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya mahakama hiyo kuitisha
jalada halisi la kesi hiyo la kujipatia dola milioni 6 za marekani, aprili 29.
Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mrembo wa
Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic, Sioi
Solomon.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro aliieleza mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu, mbele ya hakimu Mkuu Mkazi Mh. Emmillius Mchauru, kwamba
shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo, hakimu Mchauru alisema alitarajia kutoa mwenendo wa kesi hiyo,
lakini amepokea taarifa kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kwamba
washtakiwa wanatakiwa kufika mahakamani huko.
Hakimu Mchauru alisema kutokana na taarifa hiyo aliyopokea kutoka kwa
viongozi wake wa juu, washtakiwa na mawakili wao hawana budi kufika
mahakama kuu ili kujua nini kitajiri.
Mawakili wanaowatetea washtakiwa hao ni Dk.Lingo Tenga, Majura Magafu na
Alex Mgongolwa.
Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi mei 18, ambapo alisema washtakiwa
wataendelea kukaa mahabusu kama taratibu za kisheria zinavyosema, licha ya
kuitwa mahakama kuu.
Hata hivyo, baada ya kufika mahakama kuu, Jaji Mfawidhi Moses Mzuna
alisema suala ambalo lipo mbele yake linahusu taarifa ya pendekezo la kukata
rufaa ya kupinga uamuzi wa kufutwa shtaka la nane la utakatishaji fedha
lililowasilishwa na mkurugenzi wa mashtaka (DPP).
Shtaka hilo la utakatishaji fedha inadaiwa watuhumiwa wote kwa pamoja kati
ya march 2013 na septemba 2015 Jijini Dar es Salaam walitakatisha fedha dola
za kimarekani milioni sita kwa kuzihamisha kutoka katika akaunti ya kampuni
ya Egma zilizokuwa zimefunguliwa benki ya Stanbic tawi la Tanzania kwa
namba mbalimbali.
Jaji Mzuna alisema kutokana na uwepo wa taarifa hiyo mezani kwake, pande
zote mbili zinapaswa kufika siku ya alhamis mei 5, mwaka huu kwa ajili ya
kuanza usikilizwaji wa rufani.
Pia alisema licha ya kupanga tarehe hiyo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa,
endapo kama upande wa Jamhuri haujawasilisha hati ya rufani katika muda
uliotolewa, basi itatolewa taarifa ya mwenendo wa kesi hiyo.
Baada ya kutoa maelezo hayo, wakili Magafu aliieleza mahakama kwamba
wanakubaliana na hatua hiyo, licha ya kuwa upande wa Jamhuri haukufika
mahakamani hapo.
Uamuzi wa kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha, ulitolewa na
hakimu Mchauru baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi
kwamba halijakidhi vigezo vya kisheria.
Hata hivyo, uamuzi huo ulipingwa baada ya Jamhuri kupitia wakili mkuu wa
serikali, Oswald Tibabyekomya kudai kuwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP)
amewasilisha hati ya kusudio la mapendekezo ya kukata rufaa


No comments