ABC : WANATOA MIKOPO KWA RIBA NAFUU.
Meneja wa ABC Benki Tawi la Arusha akiwa kwenye banda lao katika maonyeho yaliyofanyika katika Kiwanja cha Magereza Jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kati na Kibiashara katika Kibenki Bi Joyce Malai akizungumza na wateja waliotembelea Banda la ABC Bank katika Kiwanja cha Magereza Jijini Arusha.
Bi Emma Saria ambaye ni Treasury Dearler kutoka ABC Banki akionyesha aina za Visa kadi ambazo mteja anaweza kutoa pesa kwenye ATM yeyote Duniani bila usumbufu wowote na inawemuwezesha mteja kufanya manunuzi kwa njia ya Mtandao.
NA VERO IGNATUS ARUSHA
Banki ya abac Tawi la Arusha imewataka wananchi kutokuogopa kufungua
akaunti kwani sheria ya kufungua ni rahisi ukilinganisha na benki nyingine .
Hayo yamesemwa na meneja wa Tawi la ABC Jijini Arusha Bi Mbuche Zamdi Magawa katika
maonyesho ya Utalii ya Karibu fair yaliyofanyika katika kiwanja cha Magereza
Jijini Arusha
Bi Mbuche amesema ABC Banki huwa wanamjali mteja hivyo mara zote wamekuwa
akiandaa na kufanya kile mteja anahitaji, pia kiwango cha chini cha kufungua
akaunti ni shilingi 5000 ikimlenga pia mwananchi mwenye maisha ya hali ya
chini anaweza kufungua.
Aidha ameongeza kuwa kwa upande wa wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi kwani Benki inatoa mikopo
yenye riba nafuu ambayo haitamsumbua mteja, pia kwa wateja wanaotaka
kubadilisha fedha za kigeni au wanataka kuuza fedha ,ABC Banki wanatoa
huduma hiyo kwa bei nzuri.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kati na Kibiashara za Kibenki, Bi Joyce Malai amesema kuwa
Banki inatoa Visa kadi zenye ubora wa hali ya juu inayomuwezesha mteja
kutoa pesa kwenye ATM zote duniani, na pia inaweza kumsaidia mteja kufanya
manunuzi kwa njia ya mtandao bila usumbufu wowote.
No comments