Huduma ya mabasi ya mwendo wa kasi yaanza 10 na 11 Mei 2016
Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania
imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na
mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.
Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia
maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa
barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa
barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari.
Siku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi
na moja alfajiri na saa sita mchana.
Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia
barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza
na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT
na mabasi mengine ya abiria.
Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa
huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za
BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.
No comments