Kijana Anusurika Kifo Baada Ya Kupanda na Kujirusha Kutoka Kwenye Mnara Wa Simu Jijini Mwanza
KIJANA ALIYENUSURIKA KUJIUA AKIWA AMEBEBWA.
Kijana Mmoja (pichani aliyeshikiliwa ) ambaye jina lake halikupatikana kwa
haraka, mkazi wa Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka
katikati moja ya minara wa simu iliopo jijini humo,
Tukio hilo limetokea jana na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana
huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia
mnarani hadi majira ya saa sita mchana.
Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo,
wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa
maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na
kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa
akiyatumia.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Uokoaji na Zima Moto mkoani
Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa
makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili
kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha
kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa,
ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea
morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.
Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza
fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour
Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.
No comments