David Kafulila ashindwa kesi yake dhidi ya Hasna Mwilima mahakama kuu kanda ya Tabora
DAVID KAFULILA.
Mbunge wa zamani wa Kigoma kusini (NCCR-MAGEUZI), David Kafulila
ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya
Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna
Mwilima
Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuendeshwa
chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
Katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof.
Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa
mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na
mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.

No comments