Wednesday, May 4, 2016 Kesi ya Gwajima: Wakili wa serikali Agoma kupeleka mashahidi


Upande wa Mashitaka katika kesi ya Josephat Gwajima, Askafu wa Mkuu wa
Kanisa la Ufufuo umekataa kuendelea kupeleka mashahidi wake katika
Mahahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kutaka kesi isimamishwe ili
isikilizwe rufaa yao.
Upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo notisi ya rufani tarehe 25
Aprili mwaka huu, kupinga kutopokelewa kwa ushahidi wao wa CD na picha
zilizopelekwa mahakamani hapo.
Shadrack Kimaro, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali aliiomba mahakama
kuwa, kesi hiyo isimamishwe mpaka utakapotolewa uamuzi wa rufaa ya
kupinga kukataliwa kwa ushahdi wa CD na picha zilizofikishwa mahakamani
hapo kama kielelezo cha kesi hiyo.
Shadrack amesema kuwa, ushahidi huo ulioambatana na ripoti ya mtaalamu wa
picha na barua ya ZCO iliyokwenda kwa mtaalamu wa picha, vyote vilikataliwa
mahakamani hapo.
Hata hivyo, upande wa mshtakiwa uliomba mahakama kufuta kesi hiyo
kutokana na upande wa mashitaka kukosa ushahidi na kwamba kesi haiwezi
kusimamishwa kutokana na kungojaa rufaa iliyokuwa bado haijafunguliwa.
Cyprian Mkeha, Hakimu Mfawidhi baada ya kusikiliza pande zote mbili
amesema kuwa, kesi hiyo itatajwa tena tarehe 2 Juni mwaka huu.

No comments