Kenya: Mashirika yashutumu ‘ukatili’ wa polisi


Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya yameshutumu maafisa
wa polisi wakisema walitumia nguvu kupita kiasi kukabili waandamanaji jijini
Nairobi Jumatatu.

Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu (KNHRC) imesema imeshangaza sana na
video na picha ambazo zinaenea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya
habari kuhusu yaliyojiri wakati wa maandamano hayo.

Picha hizo zinawaonesha polisi wakiwakabili waandamanaji kwa marungu.
Baadhi ya wakenya mtandaoni pia wamekuwa wakiwashutumu maafisa wa
polisi na kitambulisha mada #StopPoliceBrutality (Komesha Ukatili wa Polisi)
kinavuma Kenya.

Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Capital FM jijini Nairobi, mmoja wa
waliokabiliwa na polisi alifariki baadaye akipokea matibabu.
"Kikosi cha Polisi ni kikosi cha nidhamu na si kikosi cha kutumia nguvu. Kanuni
ziko wazi kuhusu jinsi ya kuwashughulikia raia wakati wa maandamanaji,” tume
hiyo imesema kupitia Twitter.

Mamlaka huru ya kiraia inayofuatilia shughuli za polisi (IPOA) pia imeshutumu
vitendo vya maafisa wa polisi na kusema walivuka mipaka.
Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Bw Macharia Njeru amewaambia wanahabari
kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi.

Amesema maafisa wa mamlaka hiyo wanakamilisha uchunguzi na
watawasilisha ripoti kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ili hatua
zichukuliwe dhidi ya maafisa husika.

Muungano wa upinzani CORD umekuwa ukifanya maandamano Jumatatu kila
wiki kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC)
wajiuzulu.

Viongozi wa CORD wamesema maafisa hao hawawezi kusimamia uchaguzi huru
na wa haki wakati wa uchaguzi mkuu ujao 2017.
Wameahidi kuendelea na maandamano hayo hadi maafisa hao
watakapong’atuka.ya akimshambulia raia


No comments