MWAMKO MDOGO WA WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA WAATHIRI UTALII WA NDANI .


Mwamko mdogo wa Watanzania
kutembelea hifadhi za Taifa zilizo katika
maeneo mbalimbali nchini umeathiri
kiwango cha idadi ya watu wanaotembelea
hifadhi hizo kwa mwaka hivyo kuzorotesha
mapato yanayotokana na watalii wa ndani
ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Amesema kuwa licha ya Serikali kuweka gharama ndogo za viingilio katika
hifadhi za Taifa kwa watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
bado mwamko ni mdogo hasa idadi ya watanzania wanaokwenda kutembele
hifadhi hizo jambo linalopunguza mapato yanayotokana na utalii wa ndani wa
watanzania.

Ameeleza kuwa kwa sasa watanzania kwa maana ya watu wazima
wanaotembelea hifadhi za ndani zilizoko eneo la Kaskazini hutakiwa kulipa
kiingilio cha shilingi elfu kumu (10,000) na shilingi elfu 5000 hadi 15,000
kwa hifadhi zote zilizoko kusini mwa Tanzania huku watoto wakilipia shilingi
2000 kutembelea hifadhi yoyote nchini.

Prof. Maghembe ameeleza kuwa kufuatia hali hiyo Wizara yake inaendelea na
kampeni mbalimbali ili kuwahamasisha Watanzania Wengi zaidi kushiriki
katika shughuli za utalii ndani ya nchi hivyo kuongeza patoa la Taifa.
Amesema katika kulinda na kutunza hifadhi za Taifa ili kuhakikisha zinakuwa
endelevu na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, Serikali ya
awamu ya tano imejipanga kikamilifu ujangili wa wanyama pori kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi.

Amefafanua kuwa katika kupambana na ujangili nchini Wizara kwa
kushirikiana na wadau wa uhifadhi imeshawabaini na kuwashughulikia baadhi
ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi
wanaoshirikiana na watumishi wasio waaminifu kushiriki vitendo vya ujangili
pia kuwashughulikia wawindaji haramu wanaojihusisha moja kwa moja kuua
wanyama kufanya udalali na kusafirisha wanyama hao.

Aidha, amesema kuwa katika kupambana na ujangili Serikali inaendelea
kufanya doria ili kuwashughulikia wawezeshaji ngazi ya nchi wanaonunua
nyara, kusambaza silaha, watakatishaji fedha , majangili nguli wa kimataifa
kwa kukitumia na kukiimarisha kitengo cha Intelijensia ili kiweze kutimiza
majukumu ya kiulinzi kwa ufanisi zaidi.

Pia amesema kuwa Wizara hiyo imeendendelea kuongeza idadi ya askari
wanyamapori 447 na maafisa 111 na kufanya idadi ya watumishi waliopo kwa
sasa kufikia 2,064 pamoja na kuanzisha kada nane za doria za ushirikiano
katika mifumo ya ikolojia ya Selous-Niassa-Mikumi, Ruaha- Ruangwa, Katavi
-Rukwa , Moyowosi -Kigosi, Tarangire- Manyara-Simanjiro na Ngorongoro –
Serengeti.


No comments