MAJALIWA : SEREKALI ITAHAKIKISHA INAENDELEA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI IKIWEMO URITHI WA DUNIA



NA VERO IGNATUS ARUSHA.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amesema kuwa serikali ya itaendelea kulinda na kutunza vivutio vya asili,iliwatanzania waweze kunufaika na rasilimali hizo,pamoja na kutunza na kulinda urithi wa dunia,ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya hifadhi.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo yamaendeleo endelevu unaoendelea mjini hapa ,na serikali itahakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi hifadhini,waelewe kuwepo kwa rasilimali hizo ili ziendelee kuwepo hadi kizazi kijacho kizikute.

Tanzania ni moja ya nchi  tajiri wenye urithi hivyo ili
kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi,lazima wananchi waepuke uharibifu katika maeneo ya hifadhi,ili kuongezeka uchumi na pato la Taifa na wananchi kwa ujumla."Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi
watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu kwani hata hizo maliasili ,zinatusaidia sote na hata tumewekea mikakati ya kutunza maeneo hayo ili yawe endelevu’alisema"

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni katibu Mkuu Wizara
ya Mali asili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi msema kuwa
madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo
yanatishia na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika Afrika .

Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa
miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.

Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo urithi wa dunia kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.

Aliongeza kuwa pia mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO ya
mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa
uridhi wa dunia
“Mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa Kisayansi, pia utakuwa na
manufaa kwa Taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kIutalii na kisasabali
pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi yawageni watakao
uthudhuria mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na
kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi.

Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa
na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote
za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya kufungua mkutano wa Maliasili na Unesco Jijini Arusha.

No comments