KILIFAIR:SERIKALI IPUNGUZE TOZO KUINGIA KWENYE VIVUTIO VYA UTALII.


Serikali imeombwa kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara husika  kwaajili ya kuiwezesha bodi ya utalii,kuitangaza Utalii wa Tanzania katika mataifa mabalimbali ili waweze.kuja kwa wingi kutembelea vivitio vya utalii hapa nchini .

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi na muandaaji wa maonyesho ya Kilifair ndugu Dominic Geofrey Shoo,kuwa pamoja na serikali kutenga fungu pia iangalie namna ya kupunguza tozo za kuingia kwenye vivutio vya utalii hapa nchini, kwani ipo juu ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya,Uganda,Rwanda,Zimbabwe,na Afrika ya kusini.

Muandaaji huyo wa maonyesho ya Kilifair Promotion co.Ltd. amesema kuwa kutokana na tozo kuwa kubwa wageni wengi wanalazimika kishukia nchi za jirani kufanya utalii huko,Ukizingatia kwamba Utalii ndiyo unaoliingizia Taifa pato kubwa,pia hizo nchi nyingine hawana vivutio vingi vya utalii kama hapa nchini.

Dominic ameainisha makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kuwa makampuni 261,washiriki wa ndani ya nchi 190 Makampuni kutoka nje ya nchi 71 pia wapo wanunuzi 22 kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo Ujerumani,Amerika pamoja na Asia.

"Unajua Nchi ya Tanzania ina vivutio vingi vya Asili ambavyo havijatangazwa ipasavyo ili dunia iweze kuvitambua, ili watalii waweze kuja kwa wingi hapa nchini, tunaomba serikali iweke nguvu zaidi kuwezesha bodi ya utalii kwani ni.sekta inayoingizia Taifa pato kubwa,tunaomba na tozo za kuingia hifadhini zipunguzwe ili tupate wageni wengi zaidi ,Taifa litatambulika zaidi nje na washiriki wa maonyesho pia idadi itaongezeka alisema Dominic."

Maonyesho ya Utalii ya Kilifair ni ya pili kufanyika,ya mefanyika katika Mkoani Kilimanjaro Katika manispaa ya Moshi mjini,Katika Chuo Kikuu cha Ushirika.

Kikundi cha ngoma cha Waadzabe kutoka Mkoani Singida,Wilaya ya Mkalama Kijiji cha Munguri,wakitumbuiza katika maonyesho ya Kilifair yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro Katika manispaa ya Moshi Mjini ,Katika uwanja wa chuo cha ushirika.(picha na Vero Ignatus)



Kikundi cha Baobab kutoka nchini Kenya wakitoa burudani ,katika maonyesho ya Kilifair yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro Manispaa ya Moshi,kwenye uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Altezza Climbing & Safari Athman Hasan akiwa katika maonyesho ya Kilifair katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Manispaa ya Moshi mjini,Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi mkuu wa Adventures Aloft aliyepo Katikati Ranjit Sing akiwa kwenye picha ya pamoja katika maonyesho ya Kilifair.
Afisa mauzo na masoko kutoka kampuni ya Adventures Aloft akiwa anaonyesha picha ya Baloon Camp kwenye kipepeushi.katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Mkurugenzi na muandaaji wa Kilifair Dominic Geofrey Shoo akiwa anakabidhi tuzo kwa washiriki wa maonyeshoUjumbe Ink ya utalii ya Kilifair yaliyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika

Mkurugenzi wa Baobab beach Resort iliyopo Mombasa nchini Kenya akizungumza na wageni waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya Kilifair,Katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.




No comments