Tunaitafakari Uingereza bado:Marekani
waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani
inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi.
Msimamo huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni kufuatia kura ya maoni ijumaa
wiki iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema hayo
katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond
Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo
tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema
Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini
Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.
John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo
ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano
ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo.
Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano
imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana
kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia
kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa
dunia kwa ujumla.
Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.

No comments