OSCAR PRISTORIUS KULIPA KWA ALIYOYAFANYA
Baba wa mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye aliuawa Reeva
Steenkamp, amezungumza mahakamani kwa mara ya kwanza akisema
kuwa muuaji wa Reva,
Oscar Pistorius lazima alipie yale aliyoyatenda
Akizungumza mahakamani huku amejawa na majonzi, bwana Steenkamp
alisema kuwa familia yake imetaabika kutokana na kuuawa kwa Reeva.
Alisema anaamini kuwa bintiye alikuwa amegombana na Oscar Pistorius
usiku ambao aliuawa miaka mitatu iliyopita.
Bwana Steenkamp wakati huo hakuwa na afya nzuri kuweza kuhudhuria
kesi. Mahakama mjini Pretoria itaamua hukumu ambayo itampa Oscar
baada ya hukumu ya kwanza kubadilishwa na kuwa mauaji.

No comments