KAMANDA WA POLISI JIJINI ARUSHA AKUTANA NA WADAU WA AMANI.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha
Na Vero Ignatus Arusha.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles mkumbo amewataka viongozi wa dini mkoani Arusha kuakiksha wanaubiri amani katika nyumba zao za ibada ili kuweza kuweka hali ya usalama na amani katika mkoa wa Arusha.
Wito huo ameutoa le wakati wa kongamano la siku moja la viongozi wa dini mkoani Arusha katika kongamano la viongozi wa dini mkoa arusha lilondaliwa na kamanda mkumbo na kuwashirikisha madiwani wa jiji la Arusha pamoja na viongozi wa kisiasa .
Aidha kwa upande wake meya wa jiji la Arusha kalist Lazaro akiwa kama mmojawapo wa washiriki wa kongamano hilo na kueleza kuwa ujio kongamano hilo liloandaliwa na kamanda Mkumbo ni kuonyesha mwelekeo mzuri wa kulinda amani ya Arusha.
Wakati huo huo mchungaji wa kanisa la Angilikana mchungaji Kenoni Kajembe amsema kuwa kama wao viongozi wa dini mkoani hapa wana jukumu kubwa la kuakisha kwamba dhima ya amani inajulikana kwa waumini wao wanaowaongoza.
Kongamano kama hilo linatarajiwa kufanyika mfululizo katika wilaya sita zilizobakia za mkoa wa Arusha na wiki ijayo kamanda Mkumbo anatarajiwa kufanya kongamano la amani kama hili na viongozi wa serekali za mitaa ndani ya jiji la Arusha.
Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro.
No comments