TBS:KUWEPO NA SIKU YAVIWANGO AFRIKA.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda ameyataka mashirika yanahusika na kutathimini viwango vya ubora nchini kuhakikisha wanafika katika viwanda na kwa wazalishaji wadogo wadogo ili kuweza kupata twakimu za ubora kwa usahii zaidi na kuboresha hali za bidhaa hapa nchini
Wito huo ameutoa hivi karibuni kwenye mkutano wa mashrikia ya viwango Barani Afrika ambapo shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la viwango Afrika ARSO wamezikutanisha nchi zipatazo 15 pamoja na wadau wengine kutoka mataifa ya Ulaya.
"Ni jukumu la viwango, unajua mara nyingi tumekuwa na matatizo mengi kwenye uzalishaji wa bidhaa zetu,kwenda kuwa chini ya viwango,lakini kwa utaratibhuu ambao (TBS)wameuandaa wao wenyewe,ninauhakika sasa tutakuwa na vitu vinavyokwenda na viwango,ama kiwango ambacho kipo kwenye soko,labda niombe (TBS)wawe na wasimamzi ambao wanaweza kuenea Nchi nzima ili kuhaikisha tupata bidhaa ambazo zipo kwenye viwango,alisema N'tibenda."
Mkurugenzi mkuu wa TBS Tanzania Joseph Masikitiko amesema kuwa mkutano huo ambao wanaanza kukaa kamati kuu ya viwango Afrika na baadae kufuatiwa na mkutano mkuu wa wanachama wa shirika la Viwango TBS sambamba na kuwepo na siku ya viwango Afrika.
Aidha ameongezea kusema kuwa katika mkutano huu Mashirika hayo yanatarajiwa kukaa na kutoka na maazimio ya pamoja na kupata njia maafaka za kupata bidhaa zinazolingana kwa viwango ili kuweza kupata bidhaa zinazotoka afika zenye viwango sawa.

No comments