Wabunge watatu wa CHADEMA wasimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge

Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo
(CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya
Bunge kuanzi leo kufuatia kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.

Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge
baada ya kile alichoeleza kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake.
Hata hivyo alipohojiwa kama anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi alisema kuwa
hamfahamu.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson baada
ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati hiyo
ilijiridhisha kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo kuwa ni kosa.

Aidha wabunge wangine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge ni
pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, James Ole Millya Mbunge wa
Simanjiro kwa makosa yanayofanana ya kusema uongo bungeni. Wabunge
hawa wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitano kuanzi leo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha mkutano wa
tatu wa Bunge lililokuwa na lengo la kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya
mwaka wa fedha 2016 2017. Kufuatia kuahirishwa huko, kuanzia kesho Julai
Mosi, serikali itaanza kutekeleza miradi na mpango mingine iliyoanishwa katika
bajeti hiyo.

No comments