CCM YATANGAZA SIKU YA KUMKABIDHI JPM UONGOZI.
rasmi uongozi wa chama, Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni utaratibu wa
kawaida ndani ya chama hicho. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam kwa
wanahabari, Christopher Ole Sendeka Mkutano Mkuu Maalum wa CCM
utafanyika Julai 23, 2016.
Alisema uamuzi wa kufanyika kwa mkutano huo umefikiwa baada ya Kikao
cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
kilichofanyika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Alisema
Mkutano huo Mkuu Maalum utatanguliwa na vikao vya sekretarieti, Kamati
Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa.
“…Lengo la Mkutano Mkuu huo Maalum ni kukabidhiana kijiti cha uongozi
wa juu wa chama chetu kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Dk. Kikwete
ambaye pia ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne kwenda kwa Rais wa sasa
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli
kama ulivyo utamaduni wa CCM,” alisema Ole Sendeka.

No comments