WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI WACHARUKA .



Na Vero Ignatus  Arusha.


BUNGE la Jumuiya ya Afrika Mashariki imemwagiza Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk John Magufuli kuwachukulia hatua kali Mawaziri wote
wanaohusika katika wizara zihususuzo Jumuiya hiyo kwa
kutokuhudhuria vikao vya Bunge hilo. 

Hayo yamesemwa kwa masikitiko makubwa na mwenyekiti wa kamati
ya sheria katika Bunge la Afrika Mashariki Pete Mathui kutoka Kenya, alipokuwa akielezea masikitiko
yake kuhusiana na mawaziri hao kushindwa kutimiza wajibu wao, amesema kuwa  tatizo lililopo kwa wananchi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki la kutokuijua vema Jumuiya hiyo na kutofahamishwa
mambo mengi yahusuyo Jumuiya na watu wenye wajibu huo ambao ni
Mawaziri husika.

Imebainika kuwa kutokuhudhuria kwao kwenye
vikao hivyo ndio chanzo cha wananchi wa Jumuiya hiyo kutojua
mambo mengi yahusuyo Jumuiya ya Afrika Mashariki,ambapo kwa kipindi kirefu sasa Mawaziri hao hawajatokea wala kushiriki vikao vya Bunge hilo japo wanatakiwa kufanya hivyo ili
kuweza kufikisha ujumbe kwa wananchi ambao ndio walengwa
wakubwa katika kujua mambo mbalimbali ya nchi zao.

Mathuki amedhamiria kuleta muswada katika Bunge hilo utakaoazimia
kuwakataa na kuwafukuza Bungeni hapo mawaziri wote hao ambao
kwa mujibu wake anadai wameonyesha utovu wa nidhamu kwenye
Bunge hilo.

Katika suala jingine, Mathuki amezungumzia umuhimu wa kutumia
lugha ya kiswahili katika vikao mbalimbali vya Bunge hilo ambapo pia
imeonekana ni sababu tosha kwa wananchi wengi kutojua mambo
mengi ndani ya Jumuiya kutokana na ugumu wa lugha ya kiingereza
inayotumika na kongeza kuwa inatakiwa kutumika sasa.

Amezitaka nchi zote kwa kutambua na kukienzi kiswahili wanatakiwa
kuhakikisha kinakuwa ni lugha ya kila Taifa na itumike katika
kufundishia mashuleni na hata katika matumizi .

No comments