WATU TISA WATIWA MBARONI KWA KUWAOZESHA WATOTO.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Wilson Nkambaku.
NA VERO IGNATUS ARUSHA
Watu tisa jamii ya ya kifugaji Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wametiwa mbarori kwa madai ya kuwaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo.badala ya kuwapeleka shule jambo ambalo limepelekea shule jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa upungufu wa elimu katika jamii hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Willison Nkambaku kuwa wameamua kufanya msako huo ikiwa ni moja ya kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila mwanafunzi aliyejiandikisha anakwenda shule ambapo alishirikiana na kamati yake ya ulinzi na usalama Wilaya.
Nkambaku amesema kuwa katika Wilaya yake ambayo kwa asilimia kubwa ni jamii ya wafugaji wa kimaasai wamekuwa hawapeleki watoto wao shule wanapofaulu na badala yake wamekuwa wakiwatafutia wachumba na kuwaozesha ingali wana umri mdogo hivyo kupelekea jamii hiyo kuwa nyuma kielimu.
‘’Leo tumewatia mbaroni watu tisa wakazi wa Wilaya hii ambao wamekuwa sugu kutopeleka watoto wao shule na badala yake wamekuwa wakiwaozesha na wengine kuwatafutia wachumba nah ii ni kutekeleza agizo la Rais wetu John Magufuli la kila mtoto kwenda shule’’alisema Nkambaku
‘’Mbali na hilo kuna bwana mmoja amembebesha mtoto ujauzito na kukimbilia Nchini Kenya atakamatwa tu hata akienda wapi ,na wanaume wengine wenye tabia kama hizi acheni mara moja tukiwakamata tutahakikisha tunawafunga tu’’Aliongeza Nkambaku
Aidha aliongeza kuwa msako huo utaendelea kila wakati ili kuweza kutokomeza mila potofu zinazowagandamiza watoto wa kike ambao wengi wao wana uwezo mkubwa wa darasani lakini kutokana na kunyimwa haki yao wameshindwa kupelekwa shule.
Katika hatua nyingine Nkambaku alitoa onyo kali kwa watendaji wa kata na wenyeviti ambao wamekuwa wakikumbatia taarifa mbaya ambazo zinapaswa kuripotiwa kituo cha polisi husasani kwa wananchi wanao waficha watoto wao ndani badala ya kuwapeleka shule .
‘’Wale viongozi wavijiji na kata mkibainika mnayafumbua macho yale maovu tutawasweka ndani hatutaki mzaa na baada ya hapo mtajifunza wajibu wenu ‘’alisema Nkambaku Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
Wakijibu tuhuma hizo kwa nyakati tofauti mbele ya mkuu wa Wilaya huyo juu ya sababu zilizopelekea wasiwapeleke watoto wao shule kuwa nikutokana na ugumu wa maisha waliyoyanayo.
Seleina Seuri na Lemale Mollel ni moja ya watuhumiwa ambao waliwaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo kwa madai kwamba walikoswa fedha za kuwanunulia sare za shule huku wengine wakito sababu mbalimbali ambazo hazikuwa za msingi katika suala zima la kumpatia mtoto elimu.
No comments