KIJANA EPUKA MADAWA YAKULEVYA MICHEZO NI AFYA.
Wapenzi na washabiki wa mpira wakifuatilia kwa waribu mchezo unaoendelea katika uwanja wa shule ya msingi Ngarenaro Jijini Arusha dhidi ya Timu ya Esso Star vs Timu ya Town Center.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa soka wakifuatilia mchezo unaoendelea iatika kiwanja cha shule ya msingi Ngarenaro ,hii ikiwa ni siku ya ugunguzi rasmi.
Matata Bakari mchezaji aliyeipatia timu ya Timu ya Town Center bao la kwanza ndani ya dk ya 38 dhidi ya Esso Star.
Oscar Raphael mchezaji na aliyeipatia timu ya Town Center bao la pili dk 80 ambapo timu ya Town centre iliifunga Timu ya Esso Star mabao 2 kwa bila.
Timu zote mbili siku ya uzinduzi wa ligi ya vijana iitwayo Sakina Youth Cup katika muonekano wakiwa kiwanjani wakiendelea na mchezo.
Wapenzi na washabiki wa soka wakifuatilia mchezo.siku ya uzinduzi wa ligi ya vijana iitwayo Neema Youth Club uliokuwa ukiendelea katika kiwanja cha shule ya msingi Ngarenaro hivi karibuni.
Ikiwa zimebakia siku chache kuingia kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita nakupambana na madawa yakulevya ,Jijini Arusha wamefanya uzinduzi wa Ligi ya Vijana iitwayo Neema Youth Club ikiwa nakauli mbiu "Kijana Epukana na Madawa ya kulevya."
Muandaaji wa mashindano hapo ambapo pia ni mlezi wa timu hizo bi Neema Mollel amesema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuwaondosha vijana mitaani,kuepukana na madawa ya kulevya pamoja na mambo ambayo yapo kinyume na maadili katika jamii kwa ujumla.
Aidha bi Neema.amesema kuwa mashindano hayo ni ya awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza walianza na timu 10,lakini sasa vijana wamehamasika tayari simeongezeka timu nyingine 6 na kufanya idadi iongezeke nakufikia idadi ya timu 16 hadi sasa.
Amesema kuwa timu zile za awali tayari zimeshapata uzowefu wa kutosha jambo ambalo.linawafanya vijana kuwa bize katika mazowezi,mwitikio wao ni mkubwa, huku ukisingatia michezo ni afya, ni ajira ,pia inamfanya kijana kujiongeza kiakili, kuongeza marafiki bila kusahau michezo huongeza furaha nakuondoa msongo wa mawazo kwa vijana.
Bi Neema Mollel amesema kuwa wameanza na robo fainali baadae nusu fainali hatimaye watakuja kwenye fainali yenyewe ambapo atapatikana mshindi ,ambapo fainali inatazamiwa kuchezwa ndani ya julai hivyo amewahasa wazazi na jamii.kwa ujumla kujitokeza kwa wingi.kuja kuwaona vijana wao yale wanayoyafanya ili kuwapa nguvu zaidi.
Maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya duniani huadhimishwa kila mwaka duniani kote june 26.
Bi Neema Mollel ambaye ni muandaaji wa mashindano hayo pia ni mlezi wa timu zote16,vilevile ni diwani kata ya Sakina kupitia (CCM)
No comments