Bajeti yapita kwa asilimia 100
Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali
kwa mwaka wa fedha 2016/2017 baada ya wabunge kupiga kura.
Wabunge wote waliohudhuria bungeni Jumatatu jioni walipiga kura ya ndio
wakati wa upigaji kura.
Wabunge waliopiga kura ya ndio ni 251 na wabunge ambao hawakupiga kura ni
137, Jumla ya wabunge waliopo sasa ni 389.
Mapema kabla ya Bajeti kupitishwa, Waziri wa Fedha Dk Philip Mpango
alitangaza kuwa viongozi wote wakuu wa serikali kuanzia Rais, Makamu wa
Rais na Waziri Mkuu viiunua mgongo vyao vitakatwa kodi kama ilivyo kwa
wabunge wote.
Pia wamo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wale wote waliokuwa
hawaguswi na marekebisho ya sheria (waliokuwa wakisamehewa kodi).
yagi

No comments